NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 11, 2012

Ngeleja anamuogopa Kabwe

WAZIRI wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja amemtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutoa uthibitisho wa upotevu wa  Sh2.7 trilioni. Pia amesema Serikali haiwezi kuvunja mkataba na kampuni ya kusambaza Gesi ya Pan African Energy kutokana na mkataba huo kufuata sheria.

Akizungumza na katika Mahojiano na Magic FM asubuhi jana Ngeleja alisema kinachoongelewa na Zitto ni nadharia kutokana na fedha hizo hazijathibitishwa na mtu yeyote.Alisema Kuna matatizo ya ubadhirifu katika Wizara  lakini sio kwa kiasi hicho anachokisema kutokana na kwamba hakuna kiongozi yoyote aliyethibitisha.

Alisema kama kuna mtu aliziiba fedha hizo  basi Serikali ina mkono mrefu wa kuhakikisha inawakamata wale wote walio husika. Ngeleja alisema Zitto alisema jambo hilo  kisiasa kutokana na kwamba hakutoa kidhibiti chochote kilichoonyesha kuna upotevu wa fedha hizo.

 “Hakuna upotevu huo, kinachosemwa na Zitto Kabwe ni nadharia tu,” alisema Ngeleja.
Zitto aliibua upotevu wa  wa Sh2.7 trilioni katika sekta ya madini, kutokana na ukaguzi uliofanywa  kwenye sekta hiyo na  mwaka jana na Wakala wa Ukaguzi  wa sekta ya  madini (TMAA).
 Alisema TMAA iligundua utata wa Dola1.7 bilioni katika sekta ya madini katika ukaguzi wake.
 Alisema baada ya kugundua utata huo anaomba wabunge  kuundwa kamati ili kuweza kuangalia sekta zingine ikiwemo sekta ya  gesi na mafuta ambazo zinalalamikiwa na wabunge  kupoteza fedha nyingi.

Hata hivyo Ngeleja alisema Serikali imekuwa makini kila kukicha kuhakikisha rasilimali za Taifa zinatumika kama iklivyokusudiwa na kwamba , Serikali haitaweza kuvunja mkataba kutokana na kwamba kunahitaji kukaa chini na kuweza kutafakari pamoja na kushirikisha tume ya Usuluhishi.

Alisema inawezekana kuna watendaji wabovu katika Wizara ambao tunaweza kuwaita wahalifu lakini sio kwa kiasi hicho alichokiongelea mheshimiwa Zitto.

  Ngeleja alisema kutokana  na matatizo yaliyokuwa yanalikumba Taifa ya uhaba wa umeme kwasasa kuna akiba ya umeme wa Megawati 300 baada ya kuzalisha Megawati 1028 huku matumizi yakifikia 720 kwa jana.
Alisema kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha umeme  bado Wizara haijakaa kimya  bali inashirikiana na Tanesco kuhakikisha utegemezi wa nishati ya maji unapungua .

 Alisema baada ya kujua nchi inahitaji umeme kwa wingi ndio ikaamua kuingia katika mikataba ya dharura lakini mikataba hii ndio inayowatesa watanzania kwa sasa kutokana na kwamba gharama za uzalishaji nazo hupanda.
Alisema kwa kiasi kikubwa Gharama ya umeme kwa watanzania ni kubwa klakini kutokana na  hatua hiyo, Serikali imeamua kufanya jambo hili kwa mda wa miezi sita na kwamba kama kutakuwa na marekebisho Serikali itapunguza.

“Gharama hizi za upandishaji umeme hufanyiwa baada ya miezi sita, ndio maana tunasema ni za mpito licha ya kwamba zinawatesa sana watanzania” alisema Ngeleja. Aliongeza kwamba Serikali imeaza kutoa vibali kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini ili kuweza kupewa   leseni.
Ngeleja alisema kutokana kwamba  wachimbaji wadogo kuanza kupewa leseni , Serikali imeamua kuweka vituo vya kuwasaidia wachimbaji wa madini ili kupata vifaa vya kisasa. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni pamoja na kituo kilichopo Tanga, Mwanza,  Arusha ili kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo.

 Alisema kutokana na changamoto mbalimbali za uchimbaji , aliwataka wafanyabishara wakubwa wenye uwezo kuweza kujenga kituo cha kusafishia  madini hapa nchini ili kutowa usumbufu

No comments:

Post a Comment