NJOMBE

NJOMBE

clock

Friday, February 3, 2012

Wana CCM watishia kuhamia CHADEMA

SAKATA la Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Maswa, Peter Bunyongoli, kumpiga Katibu wake,Omari Kalolo, katika kikao cha kamati ya siasa, limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wanachama wa chama hicho kutishia kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wakizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, wanachama hao walisema kitendo kilichofanywa na mwenyekiti huyo kimekifedhehesha chama, hivyo kiongozi huyo anapaswa kuwajibishwa.
Walisema kuwa vitendo kama hivyo vimekuwa vikifanywa na wahusika kufumbiwa macho na viongozi wa ngazi za juu, jambo linalowafanya wanachama kupoteza imani na chama chao na hivyo kuamua kujiunga na vyama vya upinzani.
Walisema kuwa kwa sasa watarudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA iwapo suala hilo halitachukuliwa hatua.
Akizungumzia hali hiyo kwa njia ya simu, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Adam Ngalawa, alisema suala hilo amelisikia katika vyombo vya habari na hajalipata rasmi kiofisi na hivyo kuwaomba wanachama kutulia wakati akifuatilia suala hilo.

No comments:

Post a Comment