NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

Mdee aing’ang’ania serikali mashamba yasiyotumika

MBUNGE wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA) ameibana serikali na kuitaka itoe kauli ni mikakati gani iliyonayo ili kurejesha mashamba yanayomilikiwa na wawekezaji ambayo hayatumiki.
Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza alisema kuwa kwa sasa kuna zaidi ya mashamba 14 ya mkonge yenye hekta 50 kwenye mikoa ya Morogoro na Tanga lakini hayatumiki kabisa na serikali haijatoa kauli yoyote juu ya mashamba hayo.
Mdee alisema serikali inatakiwa kutoa kauli juu ya mashamba hayo ili kubaini matumizi na kama hayatumiki ni bora yakarudishwa kwa wananchi.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, alikiri kwamba serikali inayatambua mashamba mengi zaidi.
Alisema ili kuweza kuondokana na tatizo hilo wizara imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kufuatilia mashamba ambayo hayatumiki kwa muda mrefu.
Awali katika swali la msingi Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani (CCM) aliyetaka kujua serikali inatoa kauli gani ya kuhakikisha kuwa maeneo ambayo ni mashamba ya mkonge lakini hayatumiki yanatolewa bure kwa wananchi ili wayatumie badala ya kuyaacha bila kutumiwa.
Chiza alisema kwa sasa serikali ikimaliza mchakato unaotokana na kikosi kazi, wizara itapeleka mapendekezo kwa Rais ili atoe maelekezo ya matumizi ya mashamba hayo.

No comments:

Post a Comment