NJOMBE

NJOMBE

clock

Monday, February 6, 2012

CHADEMA,CCM imeshindwa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru kwa vile hali ya ujinga na umaskini uliokuwepo kipindi hicho bado uko palepale.
Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Prof. Abdalah Safari, ndiye alitoa kauli hiyo katika mkutano wa operesheni maalumu maarufu kama ‘Ndoa CCM Mkoa wa Dar es Salaam’ uliofanyika wilaya ya Temeke, mwishoni mwa wiki.
Alisema hali ilivyokuwa katika miaka 40 iliyopita kabla hajaanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na ilivyo sasa ni vilevile haina mabadiliko ya aina yoyote, hivyo ni vema wananchi wakaiondoa CCM madarakani ili kuleta mabadiliko.
Alibainisha kuwa rasilimali nyingi za nchi zinagawiwa hovyo kwa wageni, hali inayoshangaza kwa kuwa hakuna nchi yoyote inayofanya mambo kama haya.
Kuhusu ongezeko la vifo vya wanawake na watoto, alisema vinachingiwa na saratani ya kizazi, gharama kubwa ya umeme, na hali ya kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla.
Aliishangaa CCM kutumia mabilioni ya fedha kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru ilhali wananchi hawana huduma bora za misingi kama afya, elimu na miundombinu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa CHADEMA (Bavicha), John Heche, alisema kuwa hivi sasa maisha yamepanda zaidi ya mara tatu tokea uchaguzi mkuu ulipokwisha.
Alisema kutokana na ugumu huo wa maisha, vijana wengi wameamua kucheza kamari kutokana na kukata tamaa wakingojea ukombozi.

No comments:

Post a Comment