NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

Serikali imeshindwa kusambaza maji

MBUNGE wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA), ameishambulia serikali na kudai kuwa imeshindwa kutekeleza sera ya usambazaji maji vijijini kwa muda wa miaka 50 ya uhuru.
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua ni kwa nini serikali imeshindwa kutekeleza sera ya usambazaji wa maji vijijini wakati kuna vyanzo vingi vya maji.
Silinde alisema kuwa inashangaza kuona nchi za Libya na Misiri zina maji ya kutosha licha ya nchi hizo kuwa na asili ya ukame.
Mbali na hilo alisema ni kwa nini serikali isitumie vyanzo vya maji vilivyopo kuzalisha maji ya kutosha na badala yake wananchi wamekuwa wakitaabika juu ya upatikanaji wa maji ya kutosha.
“Tatizo hili linasababishwa na ufinyu wa kibajeti lakini kwa sasa tunaagalia ni jinsi gani ya kutenga bajeti kubwa kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka ziwani.
“Mkakati wa serikali ni kuona Watanzania wanapata maji ya kutosha na wanatumia maji safi na salama bila kuwepo na shida yoyote ile,” alisema Mhandishi Rwenge.

No comments:

Post a Comment