NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

Mbunge ahoji vigezo vya kupata mkopo wa elimu

MBUNGE wa Kiwani Abdallah Haji Ali (CUF) ameitaka serikali ieleze ni vigezo gani vinavyotumika na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Kauli hiyo ameitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza swali lake la msingi ambapo alitaka kujua vigezo gani vinavyotumika na bodi hiyo kuwapatia mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema mikopo inatolewa kwa waombaji waliodahiliwa na vyuo vikuu vya elimu ya juu na ambao wanatoka shuleni moja kwa moja na wale wenye sifa kupitia mfumo wa mafunzo wa elimu ya ufundi.
Aliongeza kuwa vigezo vingine ni utaratibu wa kubaini wahitaji wa mikopo kuzingatia vigezo vinavyopimika kwa urahisi kama vile shule aliyosoma, uyatima, ulemavu na uwezo wa kiuchumi kwa mzazi.
Alisema kiwango cha mkopo kwa wale wanaostahili kukopeshwa kinategemea matokeo ya tathmini ya uwezo wa kiuchumi wa mwombaji na mzazi au mlezi kwenye vipengele vya ada ya mafunzo na mahitaji maalumu ya vitivo.
Mulugo alisema vigezo vingine ni pamoja na waombaji katika fani za ualimu wa sayansi na hisabati na sayansi na tiba hupewa mikopo kwa asilimia 100.
“Waombaji wa ualimu ambao si wa fani ya sayansi na hisabati wanapewa mikopo kwa asilimia isiyopungua 50. Huku waombaji wenye sifa linganishi katika fani ya ualimu wa sayansi na hisabati na sayansi za tiba wanapata mikopo kwa asilimia 100,” alisema

No comments:

Post a Comment