NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 18, 2012

TATHIMIN YA MBIO ZA MWENGE- MOROGORO


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Msham Abdulla Khamis aliesimama katikati akifunga mkutano wa Tathimin ya mbio za Mwenge wa Uhuru na wiki ya Vijana katika Ukumbi wa Edema Mkoano Morogoro jana .
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Kitaifa na waandaaji wa sherehe za Mwenge wakiwa kwenye tathimin ya mbio za Mwenge na wiki ya vijana wakati wa mkutano wao uliofanyika kwenye Ukumbi wa Edema Mkoani Morogoro leo wakiwa kwenye majadiliani ya kina .
Kamisaa wa Tume ya Sensa ya Taifa Mhe. Paul Kimiti akiongea na Viongozi na Waandaji wa Mbio za Mwenge Kitaifa kwenye mkutano wao wa kutathimin mbio za Mwenge uliofanyika kwenye Ukumbi wa Edema Mkoani Morogoro jana.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Msham Abdulla Khamis wa pili kulia , akiwatambulisha Wanajeshi wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ndugu Tanu Mlowezi kushoto na Mary Shayo Kulia waliofikisha Mwenge wa Uhuru kwenye Mlima Kilimanjaro, Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo mama Sihaba Nkinga wa tatu kulia wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Vijana ndugu James Kajugusi wa nne kulia na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Vijana Dkt. Steven Kissui kwenye mkutano wa Tathimin ya mbio za Mwenge uliofanyika kwenye Ukumbi wa Edema Mkoani Morogoro jana.

No comments:

Post a Comment