NJOMBE

NJOMBE

Friday, February 3, 2012

Migogoro ya wafugaji na wakulima hurudisha maendeleo nyuma

WANANCHI wa Kijiji cha Kubungo B Kata ya Doma wilayani Mvomero, wameilaumu serikali kwa kushindwa kupata suluhu ya kudumu kwenye migogoro ya wakulima na wafugaji, jambo ambalo linaendelea kuhatarisha maisha yao.
Baadhi ya wakulima walizungumzia kuendelea kuwepo kwa migogoro hiyo, kunawarudisha nyuma kimaendeleo huku kukiwa na tishio la kuibuka janga la njaa.
Wakitoa mfano wa maafa yaliyotokea mwaka 2009, mmoja wao, Ramadhani Omari, aliitaka serikali kuhakikisha maeneo yaliyobaishwa na sheria kufuatwa ili kukabiliana na tatizo hilo.
Alizitaja baadhi ya sheria zilizotungwa ikiwamo ya kulipa faini ya sh 50,000 kwa kila ng’ombe mmoja kuwa zimekuwa hazifanyiwi kazi vilivyo badala yake imekuwa mtaji wa viongozi.
Alisema pamoja na kuwapo kwa sheria hizo ndogo lakini inaonekana baadhi ya wafugaji wameendelea kukaidi sheria hizo na kuleta athari kwenye mashamba ya wakulima kwa kuharibu mazao.
Kwamba wakulima tisa; Omary Kilama, Ramadhani Omary, Mariam Abas, Saidi Ramadhani, Halima Ramadhani, Shan Ally, Tunu Drisa, Asila Kibwana na Seif Abasi, mazao yao yameliwa na ng’ombe wa mfugaji mmoja ambaye hadi leo hajakamatwa tangu Oktoba mwaka jana.
Kwa upande wake, Mtendaji wa kijiji hicho, Crispin Mfuru, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa ipo kamati ya kushughulikia migogoro hiyo ambayo inaundwa baina ya wakulima na wafugaji.

No comments:

Post a Comment