NJOMBE

NJOMBE

Monday, February 13, 2012

Mishahara ya walimu yazidi

SERIKALI imesema mishahara ya walimu imekuwa ikipanda kwa kiasi kikubwa kuliko watumishi wengine nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia alisema walimu wamekuwa wakipandishiwa mishahara kila mwaka na kwamba kiwango cha upandishaji kinatofautiana na watumishi wa kada nyingine.
Ghasia alisema katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2011, kiwango cha upandaji wa mishahara kwa walimu kimekuwa kwa asilimia 12 na 12.4 kwa mwaka, wakati kada nyingine mishahara iliongezeka kwa asilimia 5 hadi 12.6 kwa mwaka.
Majibu hayo yalitokana na swali la msingi la mbunge wa Kisarawe Seleman Jafu (CCM) ambaye alitaka kujua mpango wa serikali kushughulikia tatizo la mishahara kwa walimu ambayo imekuwa haipandi mara kwa mara na kufanya walimu wawe na ugumu wa maisha.
Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuwasaidia walimu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia vifaa vya usafiri.
Waziri alifafanua kuwa mwaka 2005, mwalimu wa daraja la tatu A’alianza na mshahara wa Sh 74,570 ambapo kwa sasa mwalimu huyo anaanza na mshahara wa sh 244,400 kwa mwezi.
Ghasia alisema walimu wa stashahada walianza na mshahara wa sh 108,800 na sasa wanaanza na sh 325,700 wakati walimu wa shahada walikuwa wakianza na mshahara wa Sh 140,000 lakini kwa sasa wanaanza na mshahara wa sh 449,200 kwa mwezi ambalo ni ongezeko la asimilia 235.14.
Kuhusu posho za walimu za kujikimu pamoja na usafiri kwa walimu wanaokwenda katika mazingira magumu, alisema serikali imeboresha mazingira yake ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo kulingana na mishahara yao.

No comments:

Post a Comment