NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 18, 2012

HAKAMA NCHINI ZATAKIWA KUTOAHIRISHA BILA SABABU ZA MSINGI

Na.Ashura Mohamed - arusha
Mahakama nchini zimetakiwa kutoahirisha kesi mara kwa mara ikiwa hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo kwa kuwa inachelewesha wahusika kupata haki zao kwa wakati.
Hali inatokana na mahakama nyngi hapa nchini kuahirisha kesi mara kwa mara bila sababu za msingi hali ambayo haileti tija kwa wenye kudai haki.
Hayo yamesemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Othman Chande wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha wanasheria Tanzania bara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa(AICC) mkoani Arusha.
Jaji chande amesema kuwa kesi zinaweza kuahirishwa ikiwa kuna sababu za msingi kama msiba au wakili ambaye yupo katika kesi hiyo ana kesi nyingine lakini sababu nyingine ambazo si za msingi zisisababishe kesi kuahirishwa ili kesi hizo zimalizike kwa wakati.
Pia Jaji chande amesema kuwa kuna changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wananchi wenye uwezo wa kawaida kupata haki yao ya msingi ya wakili pindi wanapokuwa wanakabiliwa na kesi kubwa kama ubakaji ambazo adhabu zake ni kubwa kama vile kifungo cha maisha ambapo walitakiwa kupata mtetezi lakini kutokana na mawakili wa serikali kuwa wachache wanakosa huduma hizo.
Kwa upande wake rais wa chama hicho Francis Stola amesema kuwa mkutano huo ni wa kutathimini utoaji haki na majukumu ya mahakama ambapo ameiomba serikali upande wa mahakama kutenga fungu la fedha za kutosha ili mahakimu na majaji waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi.
Hata hivyo amesema kutokana na kukosekana kwa fungu la fedha la kutosha hali hiyo inapelekea wanasheria wengi kupokea rushwa na kupelekea haki kupotea kwa wananchi ambao waniotegemea mahakama.
Aidha stola ameeleza kuwa kukosekana kwa vitendea kazi kama maktaba na kukosekana kwa vitabu vya sheria ni tatizo pindi mahakama inapotaka kutoa maamuzi.
Stola amesema mada ambazo zitakazotolewa kuwa ni pamoja na mfumo wa uendeshaji wa kesi za madai,njia gani iweze kutumika ili bunge liweze kutunga sheria ambazo zitakuwa bora,mfumo wa uwendeshaji wa kesi a jinai na nyingine nyingi.
Mkutano huo wa wanasheria kutoka Tanzania bara wameshiriki ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na mchango wao ili wananchi wenye uwezo wa chini wanapatiwa haki zao

No comments:

Post a Comment