NJOMBE

NJOMBE

Monday, February 6, 2012

Ogopeni Urais wa Makundi

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Idd, ameonya vijana nchini kutojihusisha na makundi ya wanasiasa ambao hivi sasa wako kwenye harakati za kusaka urais 2015.
Balozi Idd alitoa hadhari hiyo juzi katika kijiji cha Mtunduru, Singida Vijijini, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kuadhimisha miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Alisema kuwa makundi hayo yanayojishughulisha kutafuta urais yanapenda zaidi kuwatumia vijana, hivyo akawaomba wawe macho na makundi hayo ili yasije kuwayumbisha.
“Hawa watu wanawachanganya wananchi, wakati wa kusaka urais bado uko mbali miaka minne mbele, vijana msirubuniwe wala kuyumbishwa na watu hawa. Huu ni wakati wa kujenga nchi si muda wa kutafuta urais,” alisema.
Naye mke wa Balozi Idd, Asha Seif Iddi, aliitaka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama hicho (UWT), mkoani hapa, kuanzisha miradi mbalimbali ya uhakika, itakayosaidia kukijenga chama badala ya kutegemea misaada ya wahisani.

No comments:

Post a Comment