NJOMBE

NJOMBE

clock

Tuesday, February 14, 2012

Mnyika alalamikia vitu kupanda bei

MBUNGE wa Ubungo (Chadema) John Mnyika ameitaka Serikali  kuchukua hatua za haraka ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kutokana na ongezeko kubwa la mfumuko wa bei uliopo sasa.

Mbunge huyo aliyasema hayo  kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema  hali ngumu ya maisha iliyopo sasa inatokana na  mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu hali ambayo  ni tishio kwa uchumi na wa nchi na maisha ya wananchi.

Alisema serikali inapaswa kutambua mfumuko wa bei uliopo sasa  ni kama janga kwa taifa kwani hali hiyo inasababisha wananchi kuishi katika hali ngumu jambo ambalo linaweza kuchangia kushusha uchumi wa Taifa.

 “Kwa sasa mfumuko wa bei umeongezeka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linafanya maisha ya watanzania kuendelea kuwa magumu kwani wanashindwa  kumudu bei za bidhaa hali inayozidi kuwasababishia ugumu wa maisha,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba
“Kwa sasa serikali inatakiwa kulichukulia jambo hili kama dharura kwa kupeleka mpango wa dharura bungeni ili wabunge waweze kujadili na kulitolewa maamuzi ambao utasaidia kupunguza ugumu wa maisha kwa masilahi ya watanzania na kwa taifa ,” alisema

Alisema  mfumuko wa bei ulipo nchini unasababishwa kupunguza uzalishaji wa bidhaa za ndani jambo ambalo kwa taifa linaweza kuleta madhara makubwa kiuchumi.

“Uchumi wa taifa unaweza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kama jambo hili la mfumuko wa bei halitapewa kipaumbele kwani kwa sasa udhalishaji wa bidhaa za ndani unapungua hasa kwa bidhaa zinazotokana na kilimo,” alisema.

Alisema serikali inapaswa kuangalia kwa umakini matumizi ya fedha za serikali pamoja na  kuporomoka kwa sarafu kunatokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni pamoja na  uagizaji wa mafuta na malighafi nyingine toka nje jambo ambalo ilitawezesha  kupunguza mfumuko wa bei .

Kwa mujibu wa ripoti ya bei za bidhaailiyotolewa na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonyesha kwamba mfumuko wa bei nchini kuanzia Disemba 2011 umeongezeka hadi kufikia asilimia 19.8 ikilinganisha na asilimia 19.2 Novemba 2011

No comments:

Post a Comment