NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

Mabilioni ya JK, Karume yanufaisha 742 Zanzibar

WANANCHI 742 visiwani Zanzibar wamenufaika na mifuko ya mikopo ya maendeleo iliyotolewa kwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, ikilenga kuwaondoa katika umaskini.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Haroun Ali Suleiman, katika mkutano na waandishi wa habari jana uliofanyika Mwanakwerekwe, wilaya ya Magharibi Unguja.
Alisema kiasi cha sh bilioni 1.5 zilizotolewa katika mfuko huo zimewawezesha wananchi kujiendeleza kiuchumi na kwa kufanya miradi mbalimbali.
Waziri Haruna alisema kuwa kati ya fedha hizo, wananchi wa Unguja walikopeshwa sh bilioni moja na kurejesha milioni 15 wakati Pemba walikopeshwa sh milioni 461 na kurejesha sh milioni 11 na kufanya idadi ya sh milioni 26 ndizo zilizorejeshwa.
“Hadi kufikia sasa tayari sh milioni 18 zimesharejeshwa kati ya fedha hizo zilizokopeshwa,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa awali zoezi hilo lilizorotesha urejeshaji wake kutokana na tatizo la ufuatiliaji wa wahusika wa mikopo yenyewe.
Alisema kulikuwa hakuna ufuatiliaji na ndiyo maana hadi kufikia Desemba mwaka jana, kukawa na urejeshaji mdogo lakini sasa tatizo hilo limeondoka na kufanikiwa kukusanya sh milioni 800.
Sambamba na hilo, Waziri Haroun alisema kuwa wizara yake ina mpango wa kuanzisha mfuko maalumu wa uwezeshaji wananchi, kwa lengo la kuwaendeleza kiuchumi.
Waziri Haroun alisema kuwa mfuko huo tayari unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Aprili na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment