NJOMBE

NJOMBE

clock

Sunday, February 19, 2012

MKAZI WA SINGIDA AHUKUMIWA KUPELEKWA TAASISI YA MAGONJWA YA AKILI KWA KIPINDI CHOTE CHA MAISHA YAKE KWA KOSA LA MAUAJI.

Jaji Mwanahamisi Kwariko.
Nathanel Limu.
Mahakama kuu kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini Singida imemwamuru mshitakiwa Simon Andrew mkazi wa kijiji cha Kidaru wilayani Iramba, kupelekwa kwenye taasisi inayojishughulisha na magonjwa ya akili kwa kipindi chote cha maisha yake yaliyobakia hapa duniani.
Akitoa amri hiyo, Jaji Mwanahamisi Kwariko amesema mahakama yake imekubaliana na upande wa mashitaka kwamba mshitakiwa Simon alimuua bibi kizee Tiale Mbogo kwa kukusudia.
Aidha, Jaji Kwariko amesema mahakama pia inakubaliana na upande wa mashitaka kwamba wakati mshitakiwa Simon akitenda kosa hilo hakuwa na akili timamu.
“Mahakama hii imepokea ripoti kutoka kwa daktari kuwa mshitakiwa ni mgonjwa sugu wa afya ya akili, Kwa hali hiyo, mahakama imefiakia uamuzi kuwa mshitakiwa Simon apelekwe kwenye taasisi inayojishughulikia  watu wenye magonjwa ya akili”,amesema.
Awali mwanasheria mkuu wa serikali Neema Mwanda, alidai mbele ya Jaji Kwariko kuwa mnamo Desemba 18 mwaka 2000 katika muda usiofahamika, mshitakiwa alimuuwa kwa makusudi kikongwe Tiale Mbogo.
Neema amesema kuwa mshitakiwa Simon alikutwa na majirani wa bibi kikongwe Tiale akiwa amesimama jirani na mwili wa Tiale.
Watu hao waliweza kumkamata mshitakiwa na kumfikisha mbele ya vyombo vya dola.
Imedaiwa bibi Tiale kabla ya kufikwa na mauti hayo, alikuwa akiota jua. Mshitakiwa alimpiga na kitu ambacho hakijafahamika na kisha kufariki dunia papo hapo.

No comments:

Post a Comment