NJOMBE

NJOMBE

Thursday, July 26, 2012

Rais mpya wa Ghana kuimarisha utulivu

John Dramani Mahama aapishwa
Kiongozi mpya wa Ghana John Dramani Mahama ameahidi kuimarisha hali ya utulivu kufuatia kifo cha Rais John Atta Mills. Bw. Mahama mwenye umri wa miaka 53, aliapishwa saa kadhaa baada ya Rais aliyekuwa na umri wa miaka 68 kufariki hospitalini mjini Accra.
Upinzani wa nchini humo umesifu kasi iliyotumiwa katika kufanya mabadiliko yaliyomkabidhi Bw.Mahama mamlaka ya kuiongoza nchi ya Ghana na kusema kuwa ni kuonyesha kuwa Ghana ina upevu Kidemokrasi.
Bw. Atta Mills aliyeiongoza Ghana kuanzia mwaka 2009 alikua na saratani ya koo na alikua na mipango ya kuwania muhula wa pili katika uchaguzi unaopangwa kufanyika mwezi disemba.
Mwandishi wa BBC mjini Accra, Sammy Darko anasema kuwa Rais aliyekabidhiwa wadhifa wa Rais ataongoza kama Rais hadi wakati wa uchaguzi, ingawa haijafahamika kama atasimama kama mgombea rasmi wa chama cha NDC(National Democratic Congress.)
Wakati wa kuapishwa mbele ya kikao maalum cha Bunge kilichoitishwa kwa dharura, Bw.Mahama aliahidi kuwahudumia raia wote wa Ghana. Punde baada ya kutangazwa kuwa Rais, Bw.Mahama alitangaza maombolezi ya wiki nzima.
Kiongozi wa upinzani wa chama cha New Patriotic Party Nana Akufo Addo amesema ameahirisha kampeni za kugombea kiti cha Rais kwa heshima ya marehemu.
Mwenyekiti wa NPP Jake Obetsebi-Lamptey amesifu jinsi mabadiliko yalivyofanywa kufuatia kifo cha Rais.
Ingawa kulikuepo na mjadala mkubwa kuhusu afya ya Bw.Atta Mills, suala hilo halikugusiwa rasmi, wanaserma wandishi wa habari. Kiongozi huyo alikanusha kuhusu maumivu na kusisitiza kua katika hali nzuri ya afya.
Kulingana na msaidizi wa Rais, marehemu alilalamika kua na maumivu siku ya jumatatu jioni na tangu hapo hali yake ikazidi kua mbaya.

Wanasayansi: Ukimwi siyo tishio tena duniani

Licha ya siku chache kupata habari kuwa kunavizusi hata vya ukimwi vya ingia afrika.WANASAYANSI mbalimbali wanaoendesha tafiti mbalimbali za kutafuta tiba na chanjo ya Ukimwi, wameitangazia dunia kuwa hatua waliyofikia sasa wanauona ugonjwa huo ‘siyo hatari tena’ kwa sababu wanazo silaha zote za kuweza kukabiliana nao.

Ila wakasema, kinachowakwamisha ni ukosefu wa fedha ambazo zinahitajika katika kuendeleza tafiti na kuweka sera mpya za kukabili Virusi Vya Ukimwi (VVU) duniani.

Hayo yalibainika kwenye siku ya pili ya Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa Ukimwi unaofanyika mjini Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu zaidi 22,000 miongoni mwao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Mkutano huo na gazeti hili kufanikiwa kupata nakala yake, ilieleza kwamba jopo la wanasayansi nguli duniani walikiri kuwa wamefanyia VVU utafiti wa kutosha ndiyo maana wanatamba kuwa wamefanikiwa katika kuvidhibiti.

 “Kwa sasa tunazo silaha zote za kisayansi kumalizia mbali gonjwa hili la Ukimwi. Kilichobaki ni kutumia kikamilifu utaalamu huu katika fursa hii tuliyo nayo,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira.

Kiongozi huyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo akitokea nchini Uganda, aliongeza: “Kufanikisha hilo ni lazima tukubali kubadili mfumo kwa maana kwamba kuweka sera mpya zitakazowezesha kuokoa kundi linaloathirika zaidi na ugonjwa huu.”

Dk Katabira alifafanua: “Kinachohitajika ni kuweka mfumo utakaowashirikisha wafadhili na watunga sera katika kuweka mpango mzuri wa pamoja tuweza kulimaliza tatizo kwa silaha hizi za kisayansi.”

Naye Mtaalamu wa Tiba katika Chuo Kikuu cha California, Profesa Diane Havlir alisema: “Ujumbe wangu kwenu, hasa kwa watunga sera ni kwamba: endeleeni kuwekeza katika mipango ya kisayansi.”

Kwenye mkutano huo walishiriki pia wanasayansi wenye dawa na ushahidi unaoonyesha kuwa katika miaka ya karibuni zimeonyesha dalili nzuri za kutibu Ukimwi na kifua kikuu (TB).

Wataalamu wengi wa afya waliunga mkono kauli hiyo wakisema kwa sasa kuna uelewa mkubwa wa kitaalamu juu ya muundo na tabia ya VVU hivyo ni rahisi kwao kutengeneza dawa kwa ajili ya kuzuia, kutibu na chanjo.

Tafiti za awali
Kauli ya wanasayansi hao imekuja baada ya miaka 30 ya kipindi kigumu cha kutafiti namna ya kupata chanjo au tiba ya ugonjwa huo ambao umeua mamilioni ya watu duniani, hususan wataalamu na nguvu kazi inayohitajika kuimarisha uchumi.

Waligundua VVU mwaka 1981 na ilikuwa vigumu kupata dawa ya kuviua kwa sababu ya tabia zao na uwezo wa kujigeuza kuwa sehemu ya mwili na kutumia selikinga kuzalisha virusi wengine.
 
Wanasayansi hao walitoa kauli hizo za matumaini kukabili VVU mbele ya viongozi mashuhuri wa kisiasa, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Rais wa Ufaransa, François Hollande.

Mtaalamu anayesimamia mipango ya afya Ikulu ya Marekani, Profesa Antony Fauci, ambaye piya ni Mkurugezi wa taasisi ya nchi hiyo ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (NIAID), alikuwa miongoni mwa waliohutubia na kusifu hatua iliyofikiwa na wanasayansi duniani.

Ofisa Mkuu na Rais wa Taasisi ya Mapambano ya Ukimwi nchini Marekani,  Phill Wilson aliweka bayana kuwa pamoja na ugonjwa huo kuonekana tishio hasa kwa nchi zinazoendelea, hakuna nchi, hata zile tajiri, ambazo zinaweza kutamba haziathiriki na tatizo hilo.

Kwa hivyo akasema mikakati na sera mpya za kisayansi zinahitajika dunia nzima, hivyo akawataka wanasayansi hao ‘kuanika hadharani silaha zao’ ili zianze kutumika ulimwenguni kote.

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Mapambano ya Ukimwi (UNAIDS), Sheila Tlou aliwataka wataalamu hao kuweka mkakati mzuri utakaowezesha silaha hizo za kisayansi kuelekezwa katika nchi maskini hasa barani Afrika.

Wanasayansi hao wamekuja na kauli hizo za matumaini wakati ambapo tayari wamefanya tafiti mbalimbali na kugundua tabia za VVU ikiwa ni pamoja na vitu ambavyo vinaviwezesha kushambulia seli nyeupe za damu, maarufu kwa jina la CD4, ambazo ni sehemu ya kinga ya mwili wa binadamu.

Licha ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa kuna kila dalili ya kupatikana kwa chanjo, miaka michache iliyopita, waligundua moja ya dawa zinazotumika kupunguza makali ya VVU (ARV) ijulikanayo kama Truvada, yenye uwezo wa kumkinga mwathirika kumwambukiza mpenzi wanayeshiriki naye tendo la ndoa.

Wiki chache zilizopita, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha Truvada, ambayo ilianza kutumika sehemu mbalimbali duniani tangu mwaka 2004, kuwa ni tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomwambukiza.

Matokeo ya utafiti huo wa ARV yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa FDA, Truvada inatarajia kuanza kutumika na kusambazwa duniani katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Sheria mpya mifuko ya jamii yazua mtafaruku nchini

Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya 2012 yaliyofanywa na Bunge yamezua mtafaruku na sintofahamu, huku wafanyakazi wa sekta mbalimbali wakiyapinga kwa maelezo kwamba ni kandamizi na yanalenga kuwanyima haki ya fedha wanazokatwa kwa mujibu wa sheria kuchangia mifuko hiyo.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicolaus Mgaya aliliambia gazeti hili jana kuwa, watafungua kesi katika Mahakama ya Kazi nchini, kupinga hatua ya Serikali kubadili Sheria ya muda wa lazima wa kuchukua mafao hayo ambao ni kati ya miaka 55 na 60.

Tangu juzi watu kutoka sehemu mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakipiga simu katika chumba cha habari cha Mwananchi kwa lengo la kupata ufafanuzi wa mabadiliko hayo ya sheria yaliyopitishwa na mkutano wa saba wa Bunge, Aprili 13 mwaka huu.

Kadhalika sheria hiyo inayozuia mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii kuchukua mafao kabla ya umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55, lilichukua nafasi kubwa katika mijadala ya mitandao ya kijamii ambako wengi wa wanaliochangia, wameiponda sheria hiyo na kuiita kuwa ni ya ‘kinyonyaji’.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka alisema jana kuwa: “Hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi, maana sheria hii itafuatiwa na kanuni na miogozo mingine ambayo ninaamini kwamba itaondoa wasiwasi uliopo”.
Isaka alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika miongozo hiyo ni iwapo mwanachama atafukuzwa au kuachishwa kazi, wanachama ambao wako kwenye kazi za mikataba na wale wanaopata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini.

“Kimsingi ni kwamba suala la mafao ya kuacha kazi kabla ya umri wa kisheria wa kustaafu limefutwa kwa mifuko yote, isipokuwa katika mazingira hayo niliyoyaeleza litawekewa miongozo, na hii ni kwa faida ya wachangiaji,”alisema Isaka.

Alisema baada ya sheria hiyo kuwa imepitishwa na Bunge, kisha kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi Juni mwaka huu, SSRA ilianza mchakato wa kuweka miongozo na baada ya hapo kinachofuatia ni kutoa elimu kwa umma na baadaye kuanza kutumika kwake rasmi.

“Lakini sasa tumelazimika kuanza kutekeleza sheria hiyo mapema kuliko tulivyopanga hasa baada ya kutokea kwa suala hili kwenye public (umma) kabla ya muda tuliokuwa tumekusudia,”alisema mkurugenzi huyo.

Isaka aliongeza kuwa chimbuko la sintofahamu iliyojitokeza ni baadhi ya mifuko kuchezeana rafu kwa lengo la kupata wanachama wapya kwenye migodi na kwamba wao kama wadhibiti tayari wametoa onyo kwa mifuko iliyohusika.

“Kwanza hakuna mfuko wowote ambao una mamlaka ya kutangaza kuanza kutumika kwa sheria, ni SSRA tu wenye mamlaka hayo, kwa hiyo tumewapa onyo, kama wanajitangaza wajitangaze kwa kueleza uzuri wa mfuko wao ni siyo kuchafuana au kuchafua wengine,” alisisitiza.
Wasemavyo wafanyakazi
Mgaya alisema sheria hiyo ni kandamizi kwani inamnyima fursa mfanyakazi aliyestaafu au kufukuzwa kazi kupata malipo yake ambayo ni halali.

“Sheria hii sisi hatuikubali na tunaipinga kwa nguvu zote na tutakwenda Mahakama ya Kazi kufungua kesi ya kupinga kutumika,” alisema Mgaya na kuongeza:

“Tutafanya mawasiliano na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuwaeleza kuhusu sheria hii ili watusaidie na ikishindikana azma yetu ni kwenda mahakamani.”
Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba haiwezekani mtu anafukuzwa kazi akiwa na miaka 45 na baadhi yao hawataki tena kuajiriwa wanataka kufanyabiashara halafu unamnyima mafao yake hadi afikishe miaka 55,  kitu ambacho kitamfanya mtu huyo aishi maisha magumu.

“Sheria hiyo ingekuwa na usawa ingetumika kwa wafanyakazi wote wa Serikali na kutowabagua kama inavyojieleza kwamba, Mbunge akimaliza miaka yake mitano anachukua mafao yake. Sasa  kwa nini iwe kwao tu na si kwetu pia?,” alihoji Mgaya.

Kwa upande wao Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (Tamico) Wilaya ya Geita, kimesema kitapeleka maombi maalumu kwa Rais Kikwete kupinga marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Katibu wa Tamico Wilaya ya Geita, Benjamin Dotto alisema wameamua kupiga kura ya maoni juu ya mabadiliko ya sheria hiyo, ili wanachama wao waamue wenyewe kama wanaitaka au la.

”Tunamwomba Rais aagize kupelekwa muswada wa marekebisho bungeni, kwa ajili ya  kipengele ambacho kimeleta mtafaruku,” alisema Dotto.

Alisema kipengele cha kuzuia mfanyakazi kuchukua mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 55, kinakandamiza masilahi ya mfanyakazi mnyonge ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akichangia mapato ya nchi kupitia kodi anayokatwa.
Chimbuko la sheria
Mabadiliko ya sheria hizo za mifuko ya hifadhi ya jamii yalifanywa na Bunge Aprili 13 mwaka huu, baada ya muswada husika kuwa umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni Februari 1, 2012.

Ibara ya 107 ya muswada huo ndiyo ilipendekezwa kufutwa kwa Ibara za 37 na 44 za Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) ambavyo vilikuwa vikiruhusu mafao ya kujitoa.

Meneja uhusiano wa SSRA Sara Mssika alisema jana kuwa kufutwa kwa ibara hizo kulimaanisha kwamba hakuna mfuko wowote unaoruhusiwa kutoa tena mafao ya aina hiyo hadi hapo miongozo mipya itakapotolewa.

“Hakuna sheria ya mfuko mwingine iliyokuwa ikiruhusu mafao ya kujitoa, na kama wapo waliokuwa wakifanya hivyo, basi walikuwa wanafanya hivyo pengine kwa taratibu nyingine ambazo ni nje ya sheria za kuanzishwa kwa mifuko yao,”alisema Mssika.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni alisema lengo la marekebisho katika Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuiwezesha SSRA kufanya kazi yake kikamilifu na kusimamia na kudhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Alisema muswada huo uliandaliwa kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, wakiwamo wafanyakazi, waajiri na Serikali, pia
mifuko yenyewe kupitia vikao vya wadau na Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi Jamii na Uchumi.

“Kimsingi, wadau wote waliunga mkono mapendekezo yaliyomo katika muswada huu,” alisema Kabaka na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yatawezesha kupanuliwa kwa wigo wa wanachama kwenye mfuko kwa kuruhusu wafanyakazi wanaoingia kwenye ajira kwa mara ya kwanza ama kujiajiri wenyewe ili waweze kujiunga.
Chanzo cha Habari ni Mwananchi

Wednesday, July 25, 2012

Rais wa Ghana John Attah Mills afariki



John Atta Mills
Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata matibabu.
Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.

Ukimwi usiosikia dawa waongezeka Afrika


Dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi
Aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekuwa ukiongozeka katika bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.
Kwa muujibu wa ripoti iliyoandikwa na wataalam katika jarida la kisayansi la Lancet, hali hii imebainika baada ya watu 26,000 walioma virusi hivyo kufanyiwa utafiti.
Wataalamu hao wanasema kuwa hali hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.
Shirika moja nchini Uingereza limesema kuwa hali hiyo inazusha hofu zaidi katika bara la Afrika ambapo njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa maradhi ya Ukimwi hakuna.
Watatifi hao kutoka shirika la Afya duniani-WHO na chuo kikuu cha University College London wamegundua kuwa aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa unapatikana zaidi nchi za Afrka Mashariki.
Wataalam hao wanasema asilimia 26 % ya waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asili mia 14 katika nchi zilizo kusini mwa Afrika.
Lakini katika mataifa ya Kusini mwa Marekani , Afrika Magharibi na kati hali kama hiyo haipatikani.
Akizungumza na BBC Dr Ravindra Gupta wa shirika la UCL alisema: " virusi hivyo hambayo havisikii dawa ni kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa ipaswavyo".

Monday, July 23, 2012

Matajiri waficha fedha ng'ambo

Utafiti mpya uliofanywa sehemu mbali mbali za dunia, kutaka kujua wapi watu wanaficha fedha zao kukimbia kodi, umegundua kuwa dola kama trilioni 20, zimefichwa nchi za ng'ambo, mbali ya macho ya maafisa wanaotoza kodi.
Fedha nyingi huwekwa ng'ambo
Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa.
Dola trilioni 21 ni sawa na pato la mwaka la Marekani nzima pamoja na Japani.
Tax Justice Network inafikiri fedha zilizofichwa ng'ambo zinaweza kuwa zaidi ya hizo.
Ripoti yao inaonesha jinsi matajiri wakubwa wanavohamisha fedha na kuziweka kwenye nchi zinazoweka siri, kama Uswiswi na Visiwa vya Cayman, kwa kupitia mabenki ya kibinafsi.
Ripoti piya inaeleza kuwa nchi zenye utajiri wa mafuta, kama Urusi na Nigeria, ndio hasa kwenye mtindo wa fedha kutoweka na kuvushwa, badala ya kuwekezwa nchini.
Utafiti huo unamaliza kwa kusema wanasiasa sehemu mbalimbali za dunia, wanategemea kuwa fedha hata zikiwa kwa watu wa juu, zitavuja hatimae na kuwafikia maskini - ripoti inasema hayo hayatokei tena.

Mvua na dhoruba yaleta mafuriko Beijing

Mji Mkuu wa Uchina, Beijing, umepata mvua kubwa kabisa kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 60.
Mafuriko mjini Baijing

Watu kama 10 wamekufa, na maelfu wamehamishwa makwao.
Mvua kubwa ya jana ilifurika mabara-barani, kupeperusha mapaa, na kuporomosha miti na milingoti ya taa.
Maji mjini yalikuwa yanafika kiunoni.
Safari za ndege zaidi ya mia mbili zilivunjwa, na hivo kuwaacha maelfu ya watu wamenasa kwenye viwanja vya ndege.
Mvua sasa imeanuka mjini Beijing, lakini mvua kubwa inatarajiwa kaskazini-mashariki na kusini-magharibi mwa Uchina.

Sunday, July 22, 2012

Utoro wa wabunge wakwamisha bajeti

UTORO wa wabunge uliokemewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, wiki iliyopita jana ulikwamisha kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wiki iliyopita Makinda alisema utoro kwa wabunge hivi sasa umekithiri na akaonya kuwa kama wataendelea na tabia hiyo ipo siku watakwamisha upitishaji wa bajeti ya wizara husika.
Utabiri huo wa Spika Makinda, jana ulitimia baada ya wabunge hasa wa kambi ya upinzani kuibua hoja ya kukwamisha upitishwaji wa bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa mwaka 2012/2013 kutokana na uchache wa wabunge.
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa hoja kwa kutumia kanuni ya 112 ambapo alitaka bajeti hiyo isipitishwe kwa kuwa wabunge waliopo hawajafikia nusu ya wabunge wote.
“Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni inataka Bajeti ipitishwe ikiwa idadi ya wabunge waliohudhuria itafikia nusu ya wabunge wote.
“Hapa tulipo mimi nimeshahesabu mara mbili wabunge wote hatuzidi 110, na tunajua idadi ya wabunge wote ni 352 na nusu yake ni wabunge 175, ili tutende haki nakuomba uhesabu idadi ya wabunge waliopo kabla ya kupitisha bajeti hii ili tuwatendee haki Watanzania,” alisema.
Baada ya hapo alisimama Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) akitumia kanuni ya 77 (1) na (2) kuwa wabunge waliopo hawafikii nusu ya wabunge wote.
“Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni ya 77 (1). Akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanya maamuzi itakuwa ni nusu ya wabunge wote, kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 94 ya Katiba, isipokuwa kwamba idadi hiyo haitahusu hoja kuhusu uamuzi wa kubadilisha masharti yoyote ya Katiba kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba.
“Mbunge yeyote aliyehudhuria anaweza kumjulisha Spika kwamba, wabunge waliopo ni pungufu ya akidi inayohitajika kwa ajili ya shughuli inayoendelea.
“Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika, nasisitiza kuwa hatufiki nusu humu ndani,” alisema.
Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi) naye alisisitiza kanuni hiyo hiyo kipengele cha tatu. “Endapo Spika ataridhika kwamba kweli idadi ya wabunge walio ndani ya Ukumbi wa Bunge ni pungufu ya akidi inayohitajika basi atasimamisha shughuli za Bunge kwa muda atakaoutaja na atamwagiza katibu kupiga kengele.”
Naibu Spika Job Ndugai, alisema idadi hiyo inatakiwa wakati wa kupiga kura ya mwisho ya kuipitisha bajeti hiyo si wakati wa hatua za awali za kamati ya matumizi.
Kauli hiyo ilimfanya Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu, asimame na kutaka kiti cha Spika kisiliburuze Bunge kwa kukiuka kanuni na kuliomba Bunge liahirishe shughuli hiyo.
Hata hivyo Ndugai hakukubaliana na kauli ya Lissu. Ndugai huku akisema kuahirisha shughuli za Bunge ni gharama kubwa, alichukua muda kuamua jambo hilo.
Ndugai aliamuru Kamati ya matumizi iendelee huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alitoka nje kuwahamasisha wabunge warejee ukumbini. Mbali na juhudi za Waziri Lukuvi pia kengele ilikuwa ikipigwa nje ya ukumbi wa Bunge kuwahamasisha warejee ukumbini.
Juhudi zakwama
Pamoja na jitihada za viongozi mbalimbali wa serikali na Bunge kuhakikisha idadi ya wabunge inafika nusu, jambo hilo lilishindikana na ndipo Ndugai alipoamua kuahirisha shughuli za Bunge.
“Ni Vizuri wananchi waelewe kuwa tuna huu msiba wa kitaifa unaoendelea Zanzibar kuna wabunge wenzetu wako kule Zanzibar hasa kutoka Zanzibar kwa ruhusa ya Spika…, kuna mawaziri na manaibu wapo kule na wengine wako kule kwa shughuli maalumu.
“Kuna wabunge kadhaa ambao mimi mwenyewe nimewaruhusu wapo kwenye msiba wa mazishi ya mama wa mbunge mwenzetu, Mike Lekule Laizer (CCM).”
Wakati Ndugai akiendelea kutoa ufafanuzi huo, wabunge wa upinzani walikuwa wakitoa kauli na kugonga meza kuonesha kupinga utetezi huo.
Vitendo hivyo vilimfanya Ndugai kuwataka wamsikilize badala ya kupiga kelele ambazo haziwasaidii, kwakuwa kiti cha Spika hakiwezi kumkandamiza mtu.
“Nawaombeni ndugu zangu tunaposikilizana kama watu wazima…tupeane nafasi, mnalolitaka litakuwa …..mkisema nyinyi nawapa nafasi….mimi nikisema mnaanza kupiga kelele.
“Inanisikitisha sana tunapovunjiana heshima, tunakuwa kama watoto wadogo, mimi sidhani kama inatujengea heshima mahali popote katika nchi yetu, tunafanya jambo la msingi la taifa,” alisema.
Alisema kwa busara alizonazo ameamua kuahirisha kikao hicho, hatua ya kamati ya Bunge zima hadi Jumatatu (kesho).
Baada ya kauli hiyo wabunge wengi hasa wa upinzani walikuwa wakipiga meza kwa kushangilia ‘ushindi’ walioupata.
NCCR-Mageuzi wakomalia
Mara baada ya Bunge kumalizika wabunge wa NCCR-Mageuzi walikutana na waandishi wa habari na kuweka bayana kuwa hivi sasa wanafanya uchunguzi kujua ni vikao gani vilifanyika bila idadi ya wabunge kutimia, baada ya hapo wapeleke hoja kutaka maamuzi yaliyofikiwa yatenguliwe.
Mbunge wa Kasulu Kusini, David Kafulila, alisema maamuzi mengi yamekuwa yakifanywa bila akidi kutimia, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya taifa.
“Tutaomba Spika atupe orodha ya wabunge waliohudhuria katika kikao hiki cha Bajeti na tukibaini tutaomba maamuzi yaliyoafikiwa yatenguliwe,” alisema.
Chanzo cha habari Mtanzania Daima.

Wapinzani walalama Kilimo kupewa fedha kiduchu

KAMBI ya Upinzani Bungeni imelalamikia fedha kidogo zilizotolewa kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika katika mwaka wa fedha 2011/12.
Kambi hiyo ilisema kati ya Sh258.35 bilioni zilizoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida,  fedha za matumizi zilizopelekwa wizarani kutoka hazina kufikia Mei 31, mwaka huu ni Sh103.06 bilioni, sawa na asimilia 67.62.
Msemaji wa kambi hiyo kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Rose Kamili alisema kwa upande wa fedha za maendeleo hadi kufikia Mei 31, zilizokuwa zimepelekwa wizarani kutoka hazina ni Sh72.63 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 68.56 ya fedha zilizoidhinishwa.

“Huu ni uthibitisho kamili kwamba malengo yaliyopangwa kufikiwa mwaka wa fedha 2011/12 hayakufikiwa,” alisema Kamili alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi yake kuhusu makadirio ya matumizi ya wizara hiyo.
Aliongeza kuwa: “Serikali itoe maelezo mbele ya Bunge hili kwa nini tuipatie fedha inazoomba kwa wizara hii, wakati mwaka jana haikutekeleza bajeti iliyoidhinishwa na Bunge, hivyo kuzorotesha malengo yake.”
Alisema taarifa ya utekelezaji ya Wizara ya Kilimo, inaonyesha bajeti imepungua kutoka Sh258.35 bilioni  mwaka 2011/12 hadi Sh237.624 bilioni sawa na punguzo la asimilia 8.7.
 “Pamoja na kupungua kwa bajeti, matumizi  ya kawaida yameongezeka  kutoka Sh152.41 bilioni mwaka uliopita hadi Sh170.364 bilioni, sawa na  ongezeko la asilimia 11.78,”alisema Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) na kuongeza:
“Wakati matumizi ya kawaida yameongezeka kwa takriban asilimia 12, bajeti ya maendeleo katika wizara hii imepungua kutoka Sh105.94 bilioni mwaka 2011/12 hadi Sh67.260 bilioni ikiwa ni anguko la asilimia 57.5.”
Alisema kwa takwimu hizo ni dhahiri kwamba hakuna mkakati wa dhati wa kutekeleza kauli ya Kilimo Kwanza, kwani licha ya bajeti ya maendeleo kupungua, imeendelea kuwa tegemezi kwa fedha za nje kwa asilimia 77.7.
“Tafsiri ya utegemezi huu ni kwamba sasa Serikali imeamua kukiweka kilimo chetu rehani,” alisema

RIPOTI MAALUMU: Silaha zabadilishwa kwa gunia la mahindi

WAKATI vitendo vya uhalifu vikizidi kuongezeka sehemu mbalimbali nchini, sasa silaha kutoka nchi jirani zinadaiwa kuingia kwa wingi na kuuzwa mitaani na baadhi yake kubadilishwa na mahindi, Mwananchi Jumapili limegundua.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa, kutokana na kushamiri kwa biashara hiyo ya silaha nchini, bunduki moja aina ya Short Machine Gun (SMG) sasa inauzwa kati ya Sh300,000 hadi Sh500,000, huku bunduki aina ya AK 47 ikiuzwa kwa Sh700,000 hadi Sh1 milioni.
Wakati vijiji kadhaa mkoani Tabora vilipokumbwa na uhaba wa chakula, bunduki aina ya SMG  katika Kijiji cha Usinge wilayani Urambo  zilibadilishwa kwa gunia moja la mahindi, huku AK 47 ilibadilishwa kwa magunia mawili ya mahindi.
 Gazeti hili huko nyuma liliwahi kuripoti kuuzwa kwa bastola holela mitaani katika miji mikubwa ikiwamo Arusha, Mwanza, Moshi ambapo silaha hiyo ilikuwa ikiuzwa kati ya Sh800,000 hadi shilingi milioni moja.
Uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na Mwananchi Jumapili katika mikoa mbalimbali iliyopo mipakani umebaini kuwa, mtandao huo wa uingizaji silaha ni mkubwa na unawashirikisha matajiri na baadhi ya askari polisi wasiokuwa waaminifu.

Silaha hizo huingizwa nchini kupitia mkoani Kigoma, mpakani mwa  Rwanda, Kenya, na Burundi kwa kutumia njia mbalimbali ikiwamo, magari, pikipiki na boti kupitia Ziwa Victoria pamoja na  baiskeli ambapo bunduki hizo hufungwa kama mzigo ya kawaida.
Chanzo kimoja cha uhakika kililiambia Mwananchi Jumapili kuwa eneo la Usinge ndiyo kituo kikuu cha kupokelea silaha kutoka Burundi na Rwanda ambazo husambazwa mikoa mbalimbali nchini.

Mawakala

Mmoja wa watu ambao wamewahi kufanya biashara alisema kuwa mawakala wa silaha hizo wapo katika mikoa ya Kigoma na Tabora na kwamba ni wafanyabiashara, huku baadhi wakidaiwa kuwa watu wenye asili ya kabila la Kitutsi.
Lakini kwa Usinge alimtaja mfanyabiashara mmoja ambaye pia hukopesha fedha kwa riba (jina tunalo) ambaye inadaiwa kuwa biashara hiyo haramu anayoifanya inajulikana na mamlaka mbalimbali za juu serikalini.
Habari hizo zilieleza kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa akinunua SMG kati ya Sh300,000 hadi Sh500,000, na kwamba huzisafirisha kwa kutumia mtandao wake hadi mikoa ya Kanda ya Ziwa na huziuza kati ya Sh800,000 hadi Sh1,000,000.
Mbali na kutumia silaha hizo kwa ujambazi pia huzitumia kufanya uwindaji wa tembo  kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Habari hizo zinaeleza kuwa baada ya kuyapata meno hayo ya tembo  na kukatwa vipande, husafirisha  kwa kusaidiwa na maofisa wa maliasili na askari polisi wasiokuwa waaminifu.
Askari hao inadaiwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa kuuza meno ambapo huwalinda watu hao wanapokuwa wanasafirisha  nyara hizo huku wakiwa wamevalia sare zao za kazi.
Zinafafanua kwamba wanaposafirisha bidhaa hizo, huyaweka meno katika magunia ya mkaa kutokea Wilaya za Serengeti, Bunda, Bariadi, Maswa hadi Mwanza ambapo mtandao wa watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu huipokea mizigo hiyo na kuisafirisha kwenda kwa mawakala wa biashara hiyo.
Kwa mujibu wa vyanzo huru vya habari, silaha hizo hupokewa Mwanza ambapo huuzwa kwa wingi wilayani Serengeti kwa ajili ya kufanyia uhalifu na uwindaji wa wanyama pori.
“Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa) kwa kutumia wapelelezi wao wamejitahidi kutoa taarifa Polisi lakini wanaokamatwa baada ya muda huachiwa…,  Polisi ni chanzo kikubwa hapa,” zilieleza habari hizo.
Silaha kutokea Somalia
Inadaiwa kuwa silaha hizo zinazotokea Somalia, huingizwa nchini kwa njia ya panya kupitia Kenya kwa kutumia punda ambao huwa wanakokota mikokoteni iliyopakiwa magunia ya mahindi au karanga ambayo ndani yake huwa na silaha hizo.
Tanapa wasaka mtandao
Tangu kuuawa kwa Tembo ‘George’ maarufu kama tembo wa JK, Tanapa inadaiwa kutumia gharama kubwa kuusaka mtandao huo bila mafanikio.
Mmoja wa maofisa wa shirika hilo kwa sababu za kiusalama jina limehifadhiwa aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa anajua taarifa zote za upatikanaji wa silaha wanazozikamata.
“Kuna mambo ambayo yanatusumbua sana maana wenzetu (polisi) wanatangaza kuwa wamekamata silaha, lakini baadaye waliokamatwa huachiwa baada ya kutoa fedha,” alisema  ofisa huyo na kuongeza:
“Kama rushwa itaendelea hali ya usalama kwa mikoa ya Kanda ya Wiwa itakuwa mbaya maana silaha ni nyingi na zilizokamatwa ni kidogo kuliko zilizopo.”
Ofisa huyo alikwenda mbali zaidi kwa kufafanua kwamba baadhi ya watuhumiwa wanaouza na kusafirisha silaha hizo wana uhusiano na baadhi ya maofisa wa polisi ambao huvujisha siri kila inapofanyika operesheni ya kuwakamata watu hao.
“Matatizo yote yanachangiwana maofisa wa polisi ambao hawana mpango wa kumaliza tatizo hili hatari,  nchi itageuka dampo la silaha za kivita, vyombo vya usalama vinatakiwa kuwachunguza maofisa wanaotuhumiwa, tena wachunguzwe mpaka mali zao kwani baadhi yao  wanadaiwa kujengewa nyumba,” kilibainisha chanzo hicho.
 Kamanda Simon Sirro

Kamanda wa operesheni Tanzania, Saimoni Siro aliyeendesha msako wa watuhumiwa wa ujambazi waliohusika na mauaji ya mtalii na Meneja Msaidizi wa Kambi ya Ikoma Bush na kupora vitu mbalimbali  alikiri hivi karibuni kuwa, uingizaji wa silaha za kivita unazidi kushika kasi.
"Uhalifu wa kutumia silaha unazidi kushika kasi, wengine wanahusika na ujangili katika hifadhi na wengine kwenye matukio kama haya ya uhalifu lakini tunakabiliana nao kuhakikisha wahusika wanakamatwa, nashukuru hata wazee wamekerwa na hali hii na wanatoa ushirikiano mzuri maana nimeitwa hadi kikao cha wazee wakanieleza nao mikakati yao," alisema.
RPC Mara
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa huo, Emmanuel Lukula kwa nyakati tofauti waliliambia Mwananchi Jumapili juu ya ongezeko la silaha za kivita mkoani humo na kueleza kuwa hali hiyo inatishia usalama wa raia na mali zao, ikiwemo uwindaji haramu.
Kamanda Boaz alisema kwa kipindi cha Januari 2011 hadi Mei 2012,  bunduki  25 zimekamatwa na nyingine kusalimishwa kwa hiari ambapo kati ya hizo SMG ni 19 na Riffle 8.
Risasi zilizokamatwa ni 686 za SMG na 630 za Riffle na short gun zikiwa 56.
“Ni kweli silaha za kivita zinaingizwa nchini kutoka nchi jirani na  idadi hiyo ni kubwa na bado zipo nyingine  hazijakamatwa ila bado tunaendelea na uchunguzi kwa kuwa inaonyesha zinaingizwa kwa ajili ya kufanya uhalifu,” alisema Kamanda Boaz.

Aliongeza, “Lakini wapo wanaonunua na kudai kwamba wanazitumia  kwa ajili ya kulinda mifugo yao, lakini silaha za kivita  hairuhusiwi kumilikiwa na mtu,” alisema.Alipoulizwa kama askari nao wanahusika katika vitendo hivyo Boaz alisema,  “Ndiyo nasikia kutoka kwako, ila sina uhakika.”

Akizungumzia matukio yaliyotokea Mei mwaka huu alisema zilikamatwa bunduki nne aina ya SMG pamoja na risasi 436 ambazo ziliingizwa na watu kutoka Urambo na Kigoma na kwamba, mbili kati za  silaha hizo zilikuwa zimeishaingia wilayani Serengeti kwa mkazi mmoja wa Kijiji cha Bisarara ambaye awali alitoa risasi 228 na baada ya kubanwa akatoa nyingine.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amenunua SMG mbili na baada ya kukamatwa alitaja mtandao wake ambao mmoja wa wenzake alikamatwa mjini Magumu na mwingine Bunda.
RPC Kagera
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Salewi alikiri kuingizwa kwa silaha hizo nchini  kutoka nchi za Uganda na Rwanda na kufafanua kwamba, huingizwa kupitia njia za panya na kwamba ni vigumu kuwadhibiti watu hao.
“Ni kweli silaha zinaingizwa kwa njia ya mabasi na  boti. Eneo la mpaka wa nchi ni kubwa hivyo kuwakamata ni kazi ila juhudi zinafanyika” alisema.

Alisema silaha hizo zinatumika katika uhalifu na kuongeza, “Kwa kushirikiana na wananchi  tumekamata SMG  na AK 47 pamoja na watu wanaopeleka silaha hizo mikoa mbalimbali, wananchi wasikubali kukaa kimya wakati wakiwafahamu watu hawa.”
RPC Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,  Athumani Diwani aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa silaha hizo zinatoka nchi za Rwanda na Burundi na kwamba wanaoziingiza wanapitia mkoani Kigoma.

“Tuna changamoto kubwa kwa kuwa kasi hiyo hasa kwa mwaka jana ilikuwa kubwa, wanaingia na silaha za kivita,” alisema Diwani.
Alisema kuwa taarifa za polisi kuhusika katika matukio hayo wamezipata na wanazifanyia kazi.

RPC Kigoma
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi, Frasser Kashai aliliambia gazeti hili kwamba sababu kubwa ya kushamiri kwa vitendo vya uingizaji silaha inatokana na udhibiti mdogo katika maeneo ya mipaka ya nchi na kwamba jambo hilo linavisumbua vyombo vya ulinzi na usalama.
 “Burundi licha ya kuwa ni nchi ndogo, wameathiriwa na migogoro, jambo linalowafanya waingie nchini kutafuta hifadhi, lakini wanaingia na silaha na kufanya uhalifu huku wakisaidiwa kuhifadhiwa na wananchi,” alisema Kashai.

Alisema kuwa bunduki aina ya SMG na AK 47 ndizo zinazotumika katika uhalifu na uwindaji wa wanyama.

”Wanakuja na nia mbalimbali lakini wakiona hali siyo nzuri wanaingia katika hifadhi. Hivi sasa tunashirikiana na Tanapa kufanya msako. Tunawaomba wananchi washirikiane na Jeshi la Polisi ili kukomesha vitendo hivi,” alisema Kashai.

RPC Tabora
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (ACP) Anthony Rutha alisema watu hao wanaingiza bunduki kwa kuzipitisha porini na kwamba huingizwa na wakimbizi ambao hurudi nchini kwa maelezo ya kuja kusalimia ndugu na jamaa.

“Kambi ya Ulyanhulu inatusumbua sana kwa kuwa pale zinaingizwa silaha kali kama SMG na AK 47 na kituo chao kikubwa ni Urambo, Sikonge na hasa Usinge ambako kunatisha zaidi kutokana na kuzungukwa na mapori,” alisema.

Hata hivyo alisema kwa sasa Usinge kumetulia baada ya kituo cha polisi kufunguliwa mapema mwaka huu.

“Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Mwanza, Mara,Tabora, Shinyanga, Kigoma na Kagera ziliomba kibali  ofisi ya Waziri Mkuu ili tufanye operesheni za pamoja lakini hatujawahi kujibiwa, bila kufanya hivyo hali itakuwa mbaya.” alisema Rutha.

Rutha alisema mpaka sasa amepata taarifa kuwa baadhi ya askari wilayani Kibondo  wanahusika katika matukio hayo na kwamba jambo hilo linachunguzwa.

RPC Mwanza
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow alisema kuwa silaha hizo zinaingizwa kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi.
 “Kwa jinsi mazingira yalivyo watu hawa wanaingia nchini kwa kutumia njia za majini, barabara pamoja na njia zisizo halali jambo linalofanya vikosi vya ulinzi kushindwa kuwadhibiti watu hawa,” alisema.

Saturday, July 21, 2012

MANCHESTER UNITED WAKIWA NCHINI SOUTH AFRIKA

Anderson akiwa amembeba nyoka huku Valencia akiwa anamshangaa

Watoto wa kutoka bara la Amerika wakipiga ngoma

Valencia nae ikafika zamu yake ya kucheza na nyoka



Anderson alionekana mzoefu kuliko wenzie kwenye kucheza na Nyoka

Shinji Kagawa

Hivyi ndivyo mambo yalivyokuwa uwanja wa Taifa Simba vs TP Vita


 Mchezaji wa TP Vita Club ya DRC, akiwatoka Kigi Makasi na Kanu Mbiayavanga wa Simba
wakati wa mchezo wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki ya Kagame Cup, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya bao1-1

Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo wa Klabu Bingwa ya Afrika ya Mashariki
na Kati, kati ya timu yao na TP Vita Club ya DRC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam


Mashabiki wa Simba wakiwa wamesimama kwa dakika 1 kuwakumbuka wahanga wa ajali ya boti iliyotokea Zanzibar wiki hii

Kikosi cha Simba kilichoanza leo

Kikosi cha Vita

Sunzu akijaribu kumtoka beki wa Vita katika mechi ya leo - ambayo pia Sunzu alikosa penati.

14 wauawa katika shambulizi Marekani

Ukumbi wa Sinema mjini Denver
Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko colorado.
Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.
Alikiri kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.
Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.
Walioshuhudia tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenyen ukumbi huo mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.
Polisi wanasaema kuwa walimtia mbaroni mtu mmoja katika eneo la kuegesha magari karibu na eneo la tukio.
Alikuwa na bunduki mbili.
Wanaamini huenda silaha nyingi ziliachwa ndani ya ukumbi.
Mshukiwa huyo alisema kuwa aliacha mabomu katika nyumba yake kwenye jumba moja.
Watu wameamrishwa kuondoka kwa jumba hilo.

Friday, July 20, 2012

Shughuli ya kutafuta maiti Zanzibar

Meli ya Star Gate ikizama
Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza leo mapema huku watu miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.
Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam jana mcahan kuelekea kisiwani ikiwa imebeba watu miambili tisini.
Hadi kufikia sasa maiti 31 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.
Msemaji wa polisi nchini Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit
"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.
Siku tatu za maombolezi
Manusura walisema kuwa walihofia baadhi ya wasafiri wa meli hiyo walikwama katika meli ilipobiruka na kuanza kuzama kwa sababu ya upepo mkali.
Ali Mohamed Shein, rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa.
Ramani
Meli hiyo iliondoka Dar es Salaam saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki hapo jana ikiwa inelekea kisiwani Zanzibar.
Hamza Kabelwa, afisaa mkuu mtendaji katika idara ya hali ya hewa nchini Tranzania, aliambia BBC kuwa onyo lilitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa na hivyo vyombo vya majini havikupaswa kufanya safari zozote.
Waziri wa usafiri wa Zanzibar aliambia waandishi wa habari kuwa watalii wawili kutoka Ulaya ni miongoni mwa waliofariki.
Shughuli za uokozi zilisitishwa jana jioni kwa sababu ya dhoruba kali ya upepo.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salama,Hassan Mhelela aliambia BBC kuwa jamaa wengi wa watu waliokuwa kwenye meli hiyo walikuwa na wasiwasi na walikuwa wanajipanga kutumia ndege kwenda Zanzibar kutafuta jamaa zao.
Kivukio hicho kati ya Dar es Salaam na Zanzibar hutumiwa sana na wenyeji pamoja na watalii
Mwezi Septemba mwaka jana, takriban watu 200 walifariki baada ya meli iliyokuwa imejazana watu 800 pamoja na mizigo, kuzama huko Zanzibar.

Marekani kukabiliana na Syria bila UN


Susan Rice
Susan Rice
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Bi , Susan Rice, amesema Marekani itaimarisha juhudi zake nje ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kushinikiza serikali ya Syria kuachia madaraka.
Bi. Rice, aliyasema hayo baada ya Urussi na Uchina kutumia kura zao za turufu katika baraza hilo la Usalama kupinga vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Syria, ikiwa haitasitisha utumizi wa silaha nzito nzito dhidi ya waasi na raia.
Urussi ilisema kuwa azimio hilo la baraza la usalama lililoungwa mkono na mataifa ya Magharibi halikubaliki kwa sababu lingetekelezwa kwa kuwatumia wanajeshi.
Msemaji wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Kofi Annan, Ahmad Fawzi, alisema Bwana Annan, amesikitishwa sana na hatua hiyo ya Urussi na Uchina ya kutumia kura zao za turufu kupinga azimio hilo.
Wakati huo huo wapiganaji wa upinzani nchini Syria wameuteka na kutwaa uthibiti wa vituo kadhaa vya kuvuka mpaka kuingia nchini Iraq na Uturuki.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Iraq, amesema wapiganaji wa waasi wa Free Syrian Army, wametwaa uthibiti wa kituo kinachotumiwa kuingia nchini humo kutoka Syria.
Katika kituo kingine cha mpakani nchini Iraq, maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema wanajeshi wa waasi wamewauawa takriban wanajeshi 20 wa serikali ya Syria.
Kituo muhimu cha kuingia Uturuki kutoka Sria cha Bab al Hawa pia kilitwaliwa na waasi hao, lakini wameanza kuondoka.

Uchina kutoa dola bilioni 20 kwa Afrika


Rais wa China Hu Jinato aahidi nchi za Afrika mabilioni ya dola kwa mkopo
Rais Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Amesema kuwa mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maendeleo ya biashara.
Rais Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina na viongozi wa Afrika mjini Beijing.
Kuanzia barabara mpya za mjini Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.
Miundo mbinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani Afrika.
Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia moja na sitini hii leo.
Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia.
Baadhi ya viongozi wa mataifa ya Afrika wamefurahia uhusiano huu wakisema kuwa utakomesha tabia na hali ya kukaliwa na Mataifa ya magharibi kiuchumi na kisiasa kwa masharti yanayoambatana na mikopo hiyo.
Kwa upande mwingine Uchina imeshutumiwa na nchi za magharibi kama yenye tamaa, hali inayoifanya kupuuza haki za utu na kupendelea maendeleo ya kiuchumi na mahitaji yake ya nishati.
Mataifa ya magharibi hayajasita kuinyooshea kidole Uchina kama Mkoloni mpya wa Afrika, kwa kutangaza rekodi yake ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kuitojiingiza katika masuala ya ndani ya nchi wanakoendesha shughuli zao.
Mfano uliopo ni nchini Sudan ambako mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa uhusiano na Uchina, licha ya vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea huko Darfur.
Mashirika hayo yanaongezea kusema kuwa Uchina imesaidia katika kuchochea ghasia kupitia msaada wake wa fedha, silaha na sera.
Kwa upande wake Uchina imesisitiza kuwa itaendelea na sera yake ya kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.
Mpango wa Uchina kwa Afrika ni bayana. Ina hamu ya maliasili kutoka Bara hilo pamoja na soko la bidhaa zinazotengenezwa Uchina. Vilevile, Uchina inataka kudhibiti ushawishi wake wa kibalozi ulimwenguni kwa msaada wa Afrika.
Hivyo ndivyo hali ilivyo kuhusu miradi ya Uchina kwa Afrika ambapo watu wengi hudhani kuwa Uchina ndiyo inayodhamini miradi yote.
Benki ya Maendeleo ya Afrika, ADB huenda ikahisi kuwa Wachina wameipokonya hadhi yake kutokana na kwamba watu wengi wanaonelea hata miradi ya Benki hiyo na kudhani imedhaminiwa na Wachina, ingawaje fedha zimetoka kwenye Benki hiyo lakini wahandisi na wajenzi ni Wachina.
Viongozi wa Kiafrika hukumbushwa kuhusu mshirika wao mpya wanapokwenda Addis Ababa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.
Jengo kabambe la kisasa lililojengwa kwa vioo na mawe kwa gharama ya dola milioni 200 lilidhaminiwa na Uchina, bila shaka.

Umoja wa mataifa kushtaki Habre

Hissen Habre
Hissen Habre
Majaji katika Mahakama ya Juu zaidi ya Umoja wa Mataifa wana njia mbili wanazoweza kufuata kumsthaki aliyekuwa kiongozi wa Chad Hissen Habre, aliye uhamishoni nchini Senegal.
Wanaweza kulazimisha Senegal kumshtaki Hissene Habre kienyeji au wamhamishe hadi Ubeligiji ashtakiwe huko.
Dikteta huyo wa zamani aliyejulikana kama "Pinoche wa Afrika" amekuwa akiishi uhamishoni tangu apinduliwe mamlakani mwaka 1990.
Analaumiwa kwa kuwaua makumi ya maelfu ya watu alipokuwa akitawala Chadi kati ya mwaka 1982 hadi 1990. Amekanusha mashtaka hayo.
Habre alifikishwa katika mahakama mara ya kwanza nchini Senegal mwaka 2000 lakini mahakama za nchi hiyo zikaamua kuwa hazina mamlaka ya kusikiliza kesi yo yote dhidi yake.
Walioathirika na utawala wake waliwasilisha mashtaka dhidi ya Habre nchini Ubelgiji.
Baada ya uchunguzi wa miaka minne, Jaji mmoja wa Ubelgiji aliomba Senegal imhamishie nchini mwake.
Baada ya uamuzi huo Senegal ilikubali kuwa itamshtaki Habré katika mahakama zake lakini hatua hiyo imecheleweshwa kwa miaka sasa. Hii ni mara ya nne Ubelgiji kuomba Habre ahamishwe hadi nchini Ubelgiji. Uamuzi wa ICJ utakuwa wa mwisho.

Thursday, July 19, 2012

Juhudi za uokozi zaanza Zanzibar

Shughuli ya uokozi Zanzibar
Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina Star Gate ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.
Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.
Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
Mwandishi wa BBC mjini Dar Es Salam, Aboubakar Famau anasema kuwa meli hiyo MV Skagit ilianza kuzama saa sita saa za afrika mashariki ikiwa inaelekea bara.
Safari kati ya bara na pwani huchukua saa mbili. Inaarifiwa huenda watoto thelathini na moja walikuwa kwenye meli hiyo.
Afisaa wa usalama katika bandari ya Zanzibar alifahamisha shirika la habari la Reuters kuwa meli hiyo sasa imebiruka.
"maiti kumi na wawili pamoja na manusura kumi tayari wameodolewa baharini kufikia sasa.
Shughuli za uokozi zinaendelea ingawa kuna changamoto ya hali mbaya ya hewa." hii ni kwa mujibu wa waziri katika ofisi ya rais Mwinyihaji Makame,
Kivukio kilichoko kati ya Dar es Salaam na Zanzibar huwa na shughuli nyingi sana na huvutiwa sana na watalii pamoja na wenyeji wa Tanzania.

Waziri wa serikali wauawa Syria

Daoud Rajiha aliyekuwa shameji ya rais Bashar Al Asaad pamoja na naibu wake Assef Shawkat
Waziri wa ulinzi wa Syria pamoja na naibu wake wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga lililofanywa dhidi ya makao makuu ya ulinzi mjini Damascus.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa runinga ya kitaifa nchini Syria.
Daoud Rajiha aliyekuwa shameji ya rais Bashar Al Asaad pamoja na naibu wake Assef Shawkat walikuwa wanahudhuria mkutano wa maafisa wakuu wa serikali wakati wa shambulizi.
Afisaa mkuu wa ujasusi pamoja na waziri wa mambo ya ndani wanasemekana kuwa katika hali mahututi.
Shambulizi hili linajiri wakati taarifa zinasema kuwa waasi wanakaribia kuuzingira mji mkuu Damascus.
Shambulizi lenyewe limetafsiriwa kama hatua kubwa katika mapambano dhidi ya utawala wa rais Assad ambao wapinzani wanataka kuuangusha.
Hatua ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kuweza kupenya na kufanya shambulizi kama hili, dhidi ya makao ya ulinzi ya serikali ya Assad ambayo ulinzi wake unakuwa umedhibitiwa sana.
Eneo la shambulizi la kujitoa mhanga
Shambulizi la leo linazua maswali mengi kuhusu uwezo wa serikali kulinda maafisa wake na pia kuhusu hali ya usalama wa serikali ya Syria.
Huku idadi ya maafisa wakuu wanaojiuzulu kutoka kwa serikali ya Syria ikiongezeka, wadadisi wengi wanaamini kuwa kwa sasa hakuna nafasi kwa swali la ikiwa serikali ya Syria itaporomoka kuanzania ndani bali ni lini tu itakapoporomoka.
Wakati jeshi pamoja na zana zake nzito mfano vifaru na ndege za kivita, likiwa bado lina uwezo mkubwa wa nguvu dhidi ya upinzani, kuna dalili kuwa linakabiliwa na changamoto kubwa katika mashambulizi ya ardhini.
Hata hivyo wafuasi wa rais Assad wa madhhebu ya Alawite hawana pa kwenda. Hali hii inazua hofu ya kuchochea aapigano ya kikabila yanayoendelea nchini humo ikiwa rais Assad atangolewa madarakani.

ICC kuchunguza uhalifu wa kivita Mali

Wapiganaji wa Kiisilamu tayari kubomoa Msikiti wa Kale
Mahakama ya kimataifa ya Jinai{ICC} imeanzisha uchunguzi dhidi ya dhuluma za kivita kaskazini mwa Mali. Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hio Fatou Bensouda amesema ombi la uchunguzi huo limetolewa na serikali ya Mali.
Makundi ya waasi wakiwemo wapiganaji wa Kiisilamu yamelaumiwa kwa mauaji, ubakaji na kuwaingiza watoto jeshini.Waasi walidhibiti kaskazini mwa Mali baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Bi Bensouda amesema afisi yake imeanzisha uchunguzi wa uhalifu wa vita baada ya serikali ya Mali kukiri kwamba haina uwezo wa kuwaadhibu wanaotekeleza dhuluma hizo.Hapo mwezi jana Bi. Bensouda alisema uharibifu wa maeneo ya kale hususan katika mji wa Timbuktu utachukuliwa kama uhalifu wa vita.
Wanajeshi walipindua serikali kwa tuhuma kwamba utawala wa Mali ulishindwa kukabiliana na waasi wa Tuareg pamoja na wapiganaji wa Kiisilamu. Msukosuko wa mapinduzi ulitoa nafasi kwa makundi ya Kiisilamu na Tuareg kuyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali.
Moja ya kundi la Kiisilamu lina uhusiano na tawi la Al Qaeda Kaskazini mwa Afrika.Huku haya yakiarifiwa taasisi ya kutathmini mizozo ya kimataifa imeonya kwamba Mali inakumbwa na tisho la kungia vitani.
"International Crisis Group", limetaka pande husika katika uwongozi wa Mali na jamii ya kimataifa kuafikia suluhu la haraka kwa mzozo wa sasa.Wiki jana Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius alisema nchi yake inatafakari harakati za kijeshi kuangamiza maasi kaskazini mwa Mali.

Sunday, July 15, 2012

Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali Mkoa wa Ruvuma watembelea Mradi wa Mto Mkuju wa Uranium

 Hapo wakiwasili kambini wakipokelewa na Afisa Mazingira Bwana Robson Mshana



 Afisa usalama Bwana Nassoro Said akitoa somo juu ya usalama kazini na Mionzi
 Mgeologia Mwandamizi Bwana Roy Namgera akitoa somo juu ya shughuli nzima za utafiti
 Afisa Mazingira Bwana Robson Mshana akitoa somo juu ya mazingira na namna yanavyotunzwa na hatua zinazochukuliwa katika swala la mazingira
Meneja mahusiano Bwana Benard Mihayo akitoa ufafanuzi juu ya mahusiano ya mradi na jamii.
Hayo chini ni matukio mbalimbali walipotembelea sehemu ya maeneo ambayo yamekwishafanyiwa uchorongaji na kujionea Uranium inafananaje.







 Hapo Chini ni sehemu mbalimbali Bwana Roy akielekeza kazi mbalimbali za Shamba la sampuli




 Roy Namgera mgeologia mwandamizi akiwaelekeza namna sample zinavyohifadhiwa na kupelekwa maabara
 Mgeologia mwandamizi hapo juu akiwapimia udongo waliotokanao porini na kujui inaurani kiasi gani
 Hizi ni picha za pamoja za Viongozi hao na Baadhi ya wafanyakazi wa Mradi