NJOMBE

NJOMBE

Thursday, February 16, 2012

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr. Mohammed Gharib Bilal atembelea mradi mkubwa wa Uranium Tanzania


  Makamu wa Rais Mh.Dr.Mohammedi Gharib Bilal na Assa Mwaipopo Country manager alipowasili katika eneo la Kambi ya Mradi wa Mto Mkuju.

Makamu wa Rais Dr.Mohammed Gharib Bilal jana alitembea mkoa wa Ruvuma nakisha kutembelea mradi wa utafiti wa Uraniam mkoani hapo.Mradi huo wa utafiti wa madini ya Uranium unaojulika kama  mradi mto Mkuju uliopondani ya Mkoa wa Ruvuma,Wilayani Namtumbo katika hifadhi ya wanyama ya Selou.Mradi huo ni mradi unaomilikiwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited wanomilikiwa na Uranium One waliochini ya ARMZ.Uranium One ni Kampuni kutoka nchini Canada na ni kampuni inayojishughulisha sana na madini hayo humu ulimwenguni.ARMZ ni kampuni ya kirusi ndio inayoisimamia Uranium One na kufanya Uranium One na Mantra Tanzania Limited kuwa chini yao.
Makamu wa Rais Mh.Bilal aliweza kutembelea mradi huo kufahamishwa shughuli zinazoendelea mahali hapo.Mh Makamu wa Rais pia alionyeshwa baadhi ya mambo na shughuli zinazofanyika katika  mradi huo wa mkuju river project eneo la Nyota,Pia Mh.Bilal alielezwa kwamba utafiti huo sio kama ndio unaendelea mahali hapo tu bali bado kuna maeneo mengine ambayo Mantra Tanzania Limited imefanya utafiti na inaendelea kufanya maeneo mengine kama bonde la Mbarang’andu,Mbambabei pamoja na Bahi.
Baada ya hayo yote Makamu wa Rais Mh.Gharib Bilal alipata fursa yakuongea jambo juu ya mradi huo.Mh makamu wa Rais alisema amefurahishwa sana na mradi huo wa utafiti wa madini ya Uranium Tanzania yaliopeleka mradi huo kufika kiwango cha kufunguliwa mgodi wa madini hayo.Alisema mradi huo utakapofunguliwa na kuwa mgodi utaiweka Tanzania katika hali ya juu ya kimataifa katika uzalishaji wa madini ya Uranium,pia alizungumizia hali na mazingira ya mahali hapo kuwa nieneo zuri kwakuwa utafiti umeonyesha madini hayo hayapo mbali na sura ya dunia hivyo kufanya uchimbaji kuwa rahisi na wa gharama ndogo,Licha ya gharama za uendeshaji wa mgodi bali hata namna ya kutuza na kuweka mabaki ya udongo uliotokana na uchimbaji pia kuwarahisi na kusaidia utunzaji wa mazingira kwa kiasi kikubwa na kutokusababisha madhara kwa watu watakokuwepo eneo hilo.
Mh. Makamu wa Rais awapongeza pia Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC) kwa kazi nzuri wanayoifanya kushirikiana vizuri na Mantra Tanzania Limited katika swala zima la mionzi itokanayo na madini hayo ili kuweka hali ya usalama kwa wafanyakazi wa eneo hilo la mradi.TAEC ni taasisi ya Tanzania inayojishughulisha na mionzi,.Pia Mh. Bilal alifuraishwa sana na Kampuni ya Uranium One na ARMZ  kuisimamia kampuni ya Mantra katika mradi huo hadi hapo utakapo kuwa mgodi na kuwakaribisha katika nchi ya Tanzania wawekezaji hao kutoka Canada na Urusi na kusema mradi huo utaonyesha njia na maendeleo katika nchi ya Tanzania na mkoa wa Ruvuma na hata wilaya ya Namtumbo kwa kutoa ajira na zisizo pungua 4000 katika Tanzania.Alisema hayo kufuatia utafiti ulioonyesha kuwa madini ya Uranium katika eneo hilo ni ratili 119.4 million katika hizo 93.3 million ndio measured na indicated zipo tayari kwa uchimbaji.Pia alizungumzia kiasi cha fedha ambayo nchi  itazipata kwa maisha ya mgodi kutokana na mrahaba na kodi za wafanyakazi na mengineyo ni $ 630 million dollar,Mgodi unatarajiwa kuwa na maisha yapatayo miaka 12 pindi tu utakapo anzishwa.Mpaka sasa kinachosubiriwa ni kibali tu ili kufungua mgodi.Mh.Makamu wa Rais alisema serikali imefurahishwa sana na mradi huo hata kuwa mgodi.

Habari na Makali Machechi,Mkuju, Picha na Nurah Kalegea,Said Mateso na Makali machechi. 

Makamu wa Rais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Gharib Bilal akisalimiana na Chief Oparating Officer wa Uranium One Bw.Steve Magnuson.
             Mh.Bilal akisalimiana na Administrator wa kambi ya Mkuju River Project Bw.Peter Kaluwa                                                   
                      Makamu wa Rais akisalimiana na Manager Mausihano Bw.Benard Mihayo
                        Makamu wa Rais akisalimiana na Senior Technician Bw.Collins Salakana
                Manager Utafiti Bw.Emmanuel Nyamusika kaielezea juu ya geology ya mradi wa mto Mkuju.
Manager Mazingira Bw.John Ntukula akielezea juu ya mazingira katika eneo la mradi namna yanavyopewa kipaumbele na kutunzwa.

Afisa Usalama Bw.Nassoro Said akielezea juu ya usalama wa wafanyakazi na viumbe vinavyozunguka mradi huo.

Makamu wa Rais pamoja wengine wakielekea sehemu za maonyesho juu ya shughuli zinazoendelea katika mradi.
Afisa Usalama Bw.Nassoro Said akielezea vifaa vinavyotumika hasa katika upimaji wa mionzi katika maeneo yanayowazunguka watu.
Manager Utafiti mkuu akimwelezea Makamu wa Rais namna kazi za uchorongaji zinavyofanyika na kumwonesha baadhi ya udongo na miamba inayopatikana katika eneo la mradi.
Afisa mazingira Bw.Nurrah Kalegea akimuelezea Makamu wa Rais Mh.Bilal vifaa vinavyotumika na njia wanazotumia katika kukabiliana na swala zima la mazingira katika mradi huo.
 Afisa mazingira pia Bw.Said Mateso akielezea namna na jinsi wanavyovitumia vifaa katika kufanya kazi likiwa ni swali kutoka kwa Mh.Makamu wa Rais Dr.Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Mh.Ali Bilal katika picha ya pamoja na uongozi katika mradi wa mto Mkuju kabla ya kuondoka.
Masafara wa Makamu wa Rais Mh.Ali Bilal ukiondoka katika kambi ya Mradi wa Mto Mkuju(Mkuju River Project).

No comments:

Post a Comment