NJOMBE

NJOMBE

Monday, February 6, 2012

Chadema yazidi kuja juu Uzini

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo zikiingia siku ya saba na kuzidi kupamba moto kwa wagombea wa vyama mbalimbali katika jimbo la Uzini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelazimika kumnadi mgombea wake kwa kunukuu vitabu vya dini.
Kitendo hicho kilifanywa juzi na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Mohamed Issa, alipokuwa akimnadi mgombea wao, Ali Mbarouk Mshimba, katika Shehia ya Mchangani na Manzese.
Issa alisema wananchi hao hawana budi kumchagua ndugu yao Mshimba kwa kuwa hata katika vitabu vya dini ya Kikristo na Kiislamu vinaonyesha adhabu gani anayopaswa kupewa mtu atakayemkataa ndugu yake.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Hamad Musa Yussuf, alisema kitendo cha CCM kuwaambia wananchi wa Uzini kwamba tatizo la maji limetokana na ukosefu wa mashine ni kuwadhalilisha.
Alisema kama kweli CCM walikuwa wanawajali wananchi hao ni kwa nini wasubiri hadi kampeni ndipo wayaseme hayo na kuahidi kuwatekelezea.
Naye Ali Mbarouk Mshimba alisema endapo watamchagua, atalifanyia maendeleoa jimbo la Uzini hadi majimbo mengine yaone wivu.

No comments:

Post a Comment