NJOMBE

NJOMBE

Friday, February 10, 2012

Spika Makinda awaangukia Madaktari


SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amewaangukia  madaktari na kuwasihi waachane mgomo na badala yake warejee kazini, kuhudumia wagonjwa.Makinda alifanya hivyo jana muda mfupi baada ya kuingia katika ukumbi wa Bunge.

Kiongozi huyo wa Bunge alifanya hivyo alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu sababu za Bnge kukataa kujadili mgomo wa madaktari.

Juzi, Spika aliingia katika mgogoro na wanaharakati wakiwamo wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake,  walioaandamana kwa maelezo kuwa spika,  alikuwa ametumia ubabe kuzima hoja kuhusu mgomo wa madaktari.
Kitendo hicho kilitokana na Makinda kukataa mwongozo uliombwa na Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM) Godfrey Zambi aliyetaka bunge liache kushughulikia mambo mengine ili lijadili mgogoro huo.

“Waheshimiwa wabunge, leo (jana) Waziri Mkuu hayupo hapa amekwenda Dar es Salaam kushughulikia mgogoro wa madaktari lakini pia kamati iliyokwenda kuchunguza sakata hilo ilirudi jana (juzi) jioni sana na tulikaa pamoja na Kamati ya Uongozi hadi saa sita usiku,’’alisema Makinda.

Kamati iliyokwenda kushughulikia mgomo huo ni Kamati ya Huduma za Jamii, inayoongozwa na Magreth Sitta na ilirudi Dodoma kwa ajili ya kutoa mrejesho kwa Spika na Bunge.

“Tulipomaliza kikao usiku huo huo kamati ilinitaka mimi nizungumze na Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Rais jambo ambalo nilitekeleza usiku huo na viongozi hao walikubali kuyafanyia kazi mapendekezo yote ya kamati na leo (jana) tutaona matokeo yake,’’alisisitiza.

Alisema kamati hiyo pamoja na mambo mengine, ilibaini kuwa kulikuwa na mahusiano mabaya kati ya wizara na watumishi hao ambayo alisema yalitarajia kwisha jana .

Hata hivyo Makinda alijitetea kuwa madaktari si la kubeza hasa ikizingatiwa kuwa linabeba taswira kubwa inayogusa maisha ya watu na kwamba hali hiyo iliwaliza  wabunge waliokwenda Muhimbili.

No comments:

Post a Comment