NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, October 16, 2012

Mitambo ya kawi yashambuliwa I.Coast

Watu waliojihami wameshambulia mtambo wa kuzalisha umeme mjini Abidjan,nchini Ivory Coast.
Waziri wa kawi wa Ivory Coast, Paul Koffi Koffi,amesema kuwa watu waliokuwa wamejihami wakiwa wamevalia magwanda ya jeshi,walijaribu kuvamia mtambo wa kuzalisha umeme wa Azito mapema leo asubuhi.
Bwana Koffi Koffi alisema kuwa katika tukio lengine tofauti, watu waliokuwa wamejihami walishambulia, kituo cha polisi katika mji wa Bonoua,Mashariki mwa Abidjan.
Ivory Coast imekuwa ikilaumu wafuasi wa Rais aliyeondoka mamlakani Laurent Gbagbo kutoka nchi jirani ya Ghana kwa kufanya mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi na kambi za jeshi lake.
Bwana Gbagbo anasubiri kesi yake kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC ambapo anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji waliomtaka aondoke mamlakani na kuruhusu Rais aliyeshinda uchaguzi mwaka 2010 Alassane Ouattara, kuchukua uongozi.

No comments:

Post a Comment