NJOMBE

NJOMBE

Friday, January 18, 2013

KATIKA KUHAKIKISHA DAR ES SALAAM PANAKUWA PASAFI GREEN WSTE PRO IMEANDAA KAMPENI YA KUSHIRIKISHA WANANCHI


Katika kuhakikisha jiji la DAR ES SALAAM linakuwa safi Kampuni ya GREEN WASTE PRO imeandaa kampeni ambayo itawashirikisha wananchi na vikundi mbali mbali kushiriki katika zoezi la usafi litakalofanyika mwishoni mwa wiki
MENEJA MSAIDIZI wa kampuni hiyo ABDALLAH MBENA amesema wananchi wanahitaji elimu yak kutosha juu ya namna gani wanaweza kuweka mazingira yao safi na kwamba kwa kupitia kampeni hiyo wananchi wataweza kujinufaisha kiuchumi kupitia taka rejea na kuweka mazingira yao safi na salama.
Kwa upande wake MENEJA UENDESHAJI wa kampuni hiyo ELIZABETH SCHEEPERS amesema takataka zinafaida nyingi ikiwemo kutumia madafu kutengenezea mkaa ambao utawasaidia watanzania kuepukana na suala la ukataji miti ovyo

No comments:

Post a Comment