NJOMBE

NJOMBE

Saturday, January 14, 2012

MATITI YA LULU YAZUA BALAA CITY

Brighton Masalu na Erick Evarist
STAA kinda wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani), hivi karibuni alikumbana na kasheshe kufuatia uvaaji wake ulioacha sehemu kubwa ya matiti ikiwa wazi, Risasi Jumamosi linashusha vesi.
Tukio hilo ambalo lililowatoa udenda wanaume wakware, lilichukua nafasi Januari 11, mwaka huu ndani ya mjengo wa Mlimani City, Ubungo Jijini Dar es Salaam huku msanii huyo akionekana kutojali hali hiyo, kitendo ambacho kilizidi kuwaduwaza watu wengi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wanaume wakware walionekana kusitisha shughuli zao na kumuangalia msanii huyo kwa macho ya uchu.
Kufuatia sehemu hiyo ya kifua kuwa ‘nje nje’ inasemekana wapo wanaume waliomvaa kwa maneno yenye kuashiria kumtaka kimapenzi huku wengine wakimkejeli.
Paparazi wetu alimuuliza Lulu kama kweli siku hiyo saa kumi jioni alikuwa Mlimani City ambapo alikiri.
Aidha, alipoulizwa kama kuna sakata lilitokea kufuatia kuvaa kivazi kilichoacha matiti wazi, alishikwa na kigugumizi.
“Aaa ni kweli nilikuwa Mlimani City kufanya ‘shopping’ f’lani hivi, lakini hilo la matiti yangu kuzua balaa… aaah siwezi kusema chochote...sijui,” alisema Lulu.
Waandishi wetu walipombana zaidi juu ya uvaaji huo, Lulu hakutaka mazungumzo mengi zaidi ya kusema yeye anaona sawa. sawa.

No comments:

Post a Comment