NJOMBE

NJOMBE

Monday, January 16, 2012

Katiba mpya si mwarobaini wa shida

KATIBAmpya ijayo haitakuwa muarobani wa kutibu shida zote za wananchi kama viongozi hawatakuwa waadilifu na wazalendo kwa taifa lao.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mbunge wa Kalambo Wilayani Sumbawanga, Josephat Kandege wakati akifungua mdahalo wa kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa kupata Katiba mpya.

Mdahalo huo ulioandaliwa na muungano wa asasi zisizo za kiserikali mkoani Rukwa (Rango) na kufadhiliwa na The Foundation for Civil Society, ulifanyika katika Tarafa ya Matai wilayani humo.

Kandege aliwataka Watanzania wasitarajie kupata maendeleo endelevu kwa kupitia Katiba mpya iwapo viongozi hatakuwa waadifu na wananchi wasipokuwa wazalendo.

“Viongozi na wananchi kwa pamoja wanatakiwa kuwa waadilifu, wazalendo na watangulize maslahi ya taifa kwanza kama kweli wanataka kuona maendeleo ya kweli na ndipo hapo tutakapoona faida ya Katiba mpya tunayoisubiri kwa hamu,” alisema.

Aliwahimiza wananchi wa Kalambo kujitokeza kwa wingi mara baada ya tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya itakapoanza kufanya kazi, ili washiriki katika mchakato huo na kuacha kulalamika pasipo kuonyesha ushiriki wao.

Alisema kujitoa na kutoshiriki katika utoaji wa maoni, ni kujisaliti wenyewe kwa kuwa kutasababisha kuundwa kwa katiba isiyotatua kwa asilimia kubwa changamoto zilizopo kwenye maeneo yao.

Alilalamikia upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa kuwa Katiba ya sasa haifai na kuwakumbusha kuwa katiba hiyo wanayoibeza, ndiyo chimbuko la kutukuka kwa nchi hii.

Alitaka midahalo kama hiyo ifanyike kwa wingi ili wananchi wajiandae ipasavyo kutoa maoni
yatakayosaidia kupata katiba itakayomjali kila mmoja na kumlinda.

Pia aliwataka wananchi kutambua kuwa majadiliano ya Katiba yanapaswa kulenga maslahi ya taifa na si chama chochote cha siasa.

Naye Katibu Mtendaji wa Rango, Stanley Mshana alisema upo umuhimu mkubwa kwa makundi mbalimbali wakiwemo wazee, walemavu, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu
katika mchakacho wa kupata Katiba mpya.

No comments:

Post a Comment