NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, August 28, 2012

Hali ya hatari katika jimbo la Louisiana


Athari za kimbunga Isaac
Rais barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo la Louisiana nchini Marekani linalotishiwa na kimbunga Isaac. Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika ardhini jioni ya leo ikiwa miaka saba tangu kutokea gharika la Katrina katika eneo la New Orleans.
Kwa sasa kimbunga Isaac kimetajwa kuwa bado ni tufani japo kinatarajiwa kushika kasi zaidi na kuwa kimbunga kamili la uharibifu mkubwa inapoelekea kuvuka ghuba ya Mexico.
Kimbunga kama hicho kwa jina Katrina, kiliwaua zaidi ya watu elfu moja mia nane mjini New Orleans mnamo agosti mwaka wa elfu mbili na tano.
Tangazo hilo la hali ya hatari litawezesha afisi za serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya misaada baada ya kimbunga kupita.
Kimbunga hicho kinapiga miaka saba baada ya kimbunga kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani cha Katrina kugonga Marekani.
Chama cha Republican kimelazimika kuchelewesha kongamano lake la kitaifa , mjini Tampa, Florida kumchagua rasmi mgombea wa urais kwa chama hicho atakayepambana na rais Barack Obama.
Kimbunga saac kiliwaua watu 24 nchini Haiti na katika Jamuhuri ya Dominica na pia kusababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbea.
Hapo jana, kituo cha kitaifa cha kutabiri vimbunga, kilionya kuwa huenda kimbunga hicho kikafikia daraja ya pili kikiambatana na mawimbi makali yenye kasi ya kilomita 160, kwa saa.
Rais Obama aliitikia wito wa jimbo la Louisiana kuitaja hali kuwa ya hatari, na kuwezesha jimbo hilo kupokea msaada wa kitaifa kupambana na hali.

No comments:

Post a Comment