NJOMBE

NJOMBE

clock

Monday, January 16, 2012

Majambazi wajeruhi, waua yakipora fedha

MAJAMBAZI wanaosadikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya wakiwa na silaha za moto na mapanga wamevamia Kijiji cha Sirari na kumuua mkazi wa kijiji hicho ambaye ni raia wa Kenya
aliyefahamika kwa jina la Babu Gimonge (25).

Mtu huyo alikufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani.

Aidha kundi lingine la watu wenye silaha lilivamia katika kijiji cha Kebeyo katika Tarafa ya Inchungu na kufyatua risasi ovyo kabla ya kuingia kwenye nyumba za Magabe Robhi Nyaibaru na Matiko Nyamhanga na kuwajeruhi kwa mapanga kabla ya kupora Sh milioni 2.5.

Wakisimulia matukio hayo Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Sirari, Nyangoko Paulo alisema tukio la kuvamiwa kwa Gimonge lilitokea saa 4 usiku Jumatano Januari 12, mwaka huu.

Akimzungumzia Gimonge Mwenyekiti huyo alisema nyumba yake ilikuwa umbali wa meta 400 kutoka mpaka wa Tanzania na barabara ya Isebania nchini Kenya.

Katika tukio la pili, Diwani wa Kata ya Mbogi Servester Nyankomo alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa ambapo majambazi hao walifanya uhalifu huo kwa saa mbili katika kijiji hicho kwa kuvamia nyumba za Magabe Robhi Nyaibaru aliyeporwa Sh milioni 2 na
nyumba ya Matiko Nyamhanga aliyeporwa Sh laki tano na pia kuwajeruhi kwa mapanga.

Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Sirari, James Manyama amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema Polisi inaendelea na msako wa watuhumiwa.

No comments:

Post a Comment