NJOMBE

NJOMBE

clock

Monday, January 16, 2012

Amuua baba kwa jembe

WATU watano wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Rukwa likiwemo la mtoto kumuua baba yake kwa kumkata na jembe kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Kamilembe (40) mkazi wa kijiji cha Chonga wilayani Nkasi.

Alisema Januari 13 majira ya saa mbili usiku, Frank Kamilembe (18) anadaiwa kumuua baba yake huyo akiwa anaamulia ugomvi kati yake (Frank) na babu yake Sebastian Kamilembe (65).

Inadaiwa ugomvi huo ulitokea baada ya mtuhumiwa kumlazimisha babu yake huyo amgawie sehemu ya shamba kama urithi wake.

Katika hatua nyingine, mwanamke aitwaye Eliminata Tenganamba (32) mkazi wa kijiji
cha Sikitiko wilayani Mpanda ameuawa kwa kupigwa kwa rungu kichwani na mumewe aitwaye
Musa Moses (35).

Kwa mujibu wa Kamanda Mantage mauaji hayo yalitokea Januari 13 saa kumi jioni nyumbani kwa wanandoa hao baada ya kutokea ugomvi kati yao ambao chanzo chake bado hakijajulikana.

Kamanda Mantage alisema watuhumiwa wamekamatwa na wanatarajia kufikishwa mahakamani mara tu uchunguzi wa awali utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment