NJOMBE

NJOMBE

Saturday, January 21, 2012

CCM, CUF wapinga muswada wa mafao ya viongoziCCM, CUF wapinga muswada wa mafao ya viongozi wa kisiasa

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM na CUF wameupinga muswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa kisiasa na kusema kwamba utawabebesha wananchi wa Zanzibar mzigo mkubwa.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni ambaye pia ni Katibu wa wajumbe wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Salmin Awadh alisema wananchi wameukubali mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa matarajio makubwa ya kuimarisha hali zao za uchumi na maendeleo.

Lakini Salmin alisema kwa mujibu wa hali inavyokwenda inaonesha wazi wazi kwamba matarajio ya wananchi katika kupiga hatua ya maendeleo yameanza kuyeyuka kidogo kidogo.

“Mimi siungi mkono mswada huu kwa sababu hauna maslahi ya wananchi wa Zanzibar...huu si wakati wa kuanza kujipangiya maslahi makubwa ya viongozi wakitaifa wakati wananchi wetu hali zao ni duni,”alisema Awadh.

Mwakilishi wa Jimbo la Chonga kwa tiketi ya CUF, Abdallah Juma Abdallah yeye alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanavunja Katiba kwa sababu wanatakiwa kuupitisha mshahara wa Rais lakini kazi hiyo haifanyiw na wajumbe.

“Kwa mujibu wa Katiba, mshahara wa Rais unatakiwa kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi lakini mimi nipo mwaka wa 14 sasa sijapata kusikia kuidhinishwa kwa mshahara huo,” alisema.

Alisema wananchi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo ni ya msingi ikiwemo huduma za afya na elimu ambazo bado hazijatekelezwa kwa ufanisi. Mwakilishi wa Viti Maalumu, Raya Suleiman (CCM) alisema huu si wakati muafaka wa kupitisha mafao makubwa na manene ya viongozi wastaafu wa serikali.

“Tusubiri hadi uchumi wetu utakapokuwa mzuri na kustawi ndipo tuanze kuwekeana maslahi makubwa ya mafao ya viongozi wastaafu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Raya.

Imeandikwa na Khatib Suleiman

No comments:

Post a Comment