NJOMBE

NJOMBE

Monday, January 16, 2012

Maji nayo kupanda

SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ( E W U R A ) kukubaliana na
Tanesco na kutangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 40.29, sasa ni zamu ya Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco).

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji zinasema gharama za maji zitapanda kunatokana na kupanda kwa gharama za umeme.

Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala, ametangaza kusudio hilo la kupandishwa kwa gharama za huduma ya majisafi na majitaka.

Midala alisema hayo juzi akiwa Bomu wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, katika mtambo wa kusafisha na kusafirisha maji wa Ruvu Chini alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi.

Midala alisema ongezeko hilo la bei litaongeza gharama za uzalishaji wa majisafi na majitaka
na hivyo kuifanya Dawasco ilazimike kuwapandishia bei ya huduma ya majisafi wateja wake.

Midala hakusema bei ya huduma hiyo itaongezeka kwa kiasi gani, kutokana na Dawasco na
mamlaka zingine za majisafi na majitaka nchini kutojipangia bei za huduma hiyo.

Aidha, Midala alieleza kuwa mwishoni mwa mwaka jana, Dawasco ilipendekeza bei mpya za huduma ya majisafi na kuwasilisha mapendekezo hayo Ewura. Hata hivyo Ewura hawakukubaliana na mapendekezo hayo.

No comments:

Post a Comment