NJOMBE

NJOMBE

Saturday, January 14, 2012

DOGO JANJA ANAMAMBO MAKUBWA


Rehema Fabian
Na Shakoor Jongo
MSHINDI wa shindano la kumsaka Balozi wa Kiswahili Bongo mwaka 2009, Rehema Fabian (pichani), anadaiwa kwenda Manzese, Dar anakoishi msanii Abdulaziz Abubakar Chende ‘Dogo Janja’ na kumtorosha, Risasi Jumamosi ndilo lenye picha nzima.
Akifunguka juzikati jijini Dar, mlezi wa Dogo Janja ambaye pia ni Rais wa Manzese na Kundi la Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’ alisema Rehema alifanya kosa hilo hivi karibuni na kwamba limemsikitisha sana.
Alisema siku ya tukio, alirudi nyumbani saa tisa usiku na kumkosa msanii huyo, alipouliza akajibiwa alifuatwa na demu mmoja ambaye mara nyingi huwa beneti na Tundaman (Rashid Ramadhan).
Madee alisema kuwa alipomuuliza Tundaman ni demu gani huwa naye beneti mara nyingi, alimjibu kuwa ni Rehema Fabian.
“Aliponiambia hivyo nilianza kuwasaka, nikasikia wapo viwanja, sijui wapi huko! Niliingia mtaani kuwatafuta lakini sikuwaona,” alisema Madee.
Aliongeza kuwa kibaya zaidi, yeye ndiye aliyekabidhiwa dogo huyo kutoka kwa wazazi wake, Arusha.
“Mimi ndiye niliyekabidhiwa Dogo Janja, nakaa naye, lolote litakalomtokea nitaulizwa mimi,” alisema.
Akaongeza: “Sasa kwa mfano katika safari yao wangepata ajali, nani angeulizwa? Halafu mlango waliuacha wazi. Kwa kweli siwezi kumvumilia, nitahakikisha namfunza adabu (Dogo Janja), nikishindwa namrudisha kwao Arusha.”
Kwa upande wake, Rehema alisema si kweli kuwa alimtorosha Dogo Janja, bali anachokumbuka  dogo huyo alimpigia simu akimtaka ampe ofa ya kwenda kumlipia kwenye ‘swimming pool’ ili aogelee.
“Lakini kwa vile nilikuwa bize sikumfuata, nashangaa kutuhumiwa eti nilikwenda kumtorosha,” alisema Rehema.
Akasema: “Unajua Dogo Janja ana mambo makubwa, inawezekana kuna mwanamke mwingine alikwenda kumtorosha alipobanwa akanitaja mimi. Mimi nikimtaka nitamuomba Madee lakini siwezi kumtorosha, labda kuna mengine yamejificha.”

No comments:

Post a Comment