NJOMBE

NJOMBE

clock

Friday, January 20, 2012

Huwezi Amini Huyu ni Mwanaume Aliyejigeuza Mwanamke

Oneal Morris mwanaume aliyebadilisha jinsia yake kuwa mwanamke Kwa haraka haraka au bila kuambiwa unaweza kuamini kabisa kuwa huyu kwenye picha ni mwanamke mwenye makalio makubwa kama ya wale wanawake waliojidunga sindano za wachina, lakini cha kustaajabisha huyu ni mwanaume aliyebadilisha jinsia yake kuwa mwanamke na baadae kuongeza makalio yake.
Akiwa amefikishwa kituo cha polisi cha Florida nchini Marekani na kusimamishwa wima ili apigwe picha za jalada la kesi yake, Oneal Morris anaonekana kwa umbile hana tofauti na mwanamke.

Oneal alikuwa ni mwanaume ambaye miaka michache iliyopita alijibadilisha jinsia yake kuwa mwanamke na kisha baadae kuongeza homoni za kike na kujidunga sindano za kuongeza makalio yake.

Oneal ambaye ana umri wa miaka 30, alifikishwa kituo cha polisi kutokana na kuanzisha zahanati bubu ambapo alikuwa akiwadunga sindano za kuongeza makalio wanawake ambao walitaka kuwa na makalio makubwa kama kina Jennifer Lopez au Kim Kardashian.

Oneal anakabiliwa na mashtaka ya kumdunga sindano ya kuongeza makalio mwanamke ambaye alidhurika na sindano hizo na matokeo yake kuwahishwa hospitali ambako hadi sasa amelazwa kwenye chumba cha watu mahututi.

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa sindano alizotengeneza Oneal zilikuwa na vitu vingi ambavyo ni sumu katika mwili wa binadamu. Miongoni mwa vitu vilivyotumika kutengeneza sindano hiyo ya kuongeza makalio ni simenti, gundi ya super-glue na mafuta ya gari.

Oneal anakabiliwa na mashtaka ya kutoa huduma za kidaktari bila ya kuwa na leseni na pia kutengeneza sindano ambazo hazijathibitishwa na watalaamu wa madawa.

No comments:

Post a Comment