SERIKALI inawachunguza baadhi ya maofisa wake waandamizi kwa tuhuma za
wizi wa dola50 milioni za Marekani sawa na Sh86 bilioni, zilizotengwa
kwa ajili ya ununuzi wa mafuta mazito ya kuzalishia umeme kwa Kampuni
ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), katika kipindi hiki nchi
inapokabiliana na tatizo la uhaba wa nishati hiyo.
IPTL
inayozalisha megawati 100 za umeme iliingia mkataba na Shirika la Umeme
Tanzania(Tanesco), lakini utendaji wake umekuwa na mkanganyiko.Chanzo
kutoka serikalini kililiambia gazeti dada la The East African la
Februari 12, kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba baadhi ya maafisa
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Hazina na Tanesco, wanahusika
katika mpango huo wa wizi.
Waziri wa Nishati na Madini William
Ngeleja alipoulizwa alijibu, “Ndiyo naweza kuthibitisha upo uchunguzi
unaoendelea, lakini ndiyo kwanza upo katika hatua za awali.” Tayari
taarifa za awali za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali (CAG), zinaonyesha kumekuwa na maelezo yaliyokiuka utaratibu wa
fedha zilizolipwa na Serikali kwa ajili ya usambazaji wa mafuta mazito
kutoka kampuni za ndani.
Ukosefu wa nishati ya umeme unaoikabili
nchi kwa sasa unaifanya Tanesco kulipa IPTL dola12 milioni za Marekani
sawa na Sh19.2 bilioni kila mwezi, kwa uzalishaji wa megawati 60 badala
ya megawati 100.
Mwaka 1995, Tanesco iliingia mkataba na
IPTL, mkataba ambao uliihusisha kampuni ya nchini Malaysia , Mechmar
Corporation na wawekezaji wa ndani, na VIP Engineering and Marketing
Company kwa ajili ya kuzalisha megawati 100 kwa kutumia mitambo
inayotumia dizeli kwa miaka 20.Katika mkataba huo, VIP ina hisa ya
asilimia 30 na ile ya Mechmar ya Malaysia ikiwa na hisa ya asilimia
70.Serikali ilikubali kulipa kwa ajili ya uzalishaji huo kwa kuwa
haikuwa na njia nyingine.
Mpango wa kuifilisi IPTLTayari hivi
karibuni Mahakama iliamua IPTL ifiilisiwe na jukumu hilo lilikabidhiwa
kwa Wakala wa Ufilisi, Vizazi na Vifo (Rita).Hata hivyo, baadhi ya benki
zinazoidai IPTL ziliweka zuio mahakamani zikitaka kwanza kulipwa fedha
zao ambazo kampuni hiyo ilikopa.IPTL inakadiriwa kuwa na Sh200 bilioni
zilizopo Benki Kuu (BoT) ambazo kama ikifilisiwa zingeangukia mikononi
mwa Serikali. Kampuni hiyo imekuwa ikiitafuna Tanesco mabilioni ya
shilingi tangu kuingia mkataba huo ambao umekuwa ukitajwa kama wa
kifisadi, kuliko hata wa Richmond.
No comments:
Post a Comment