MBUNGE wa Ubungo (Chadema) John Mnyika ameitaka Serikali kuchukua
hatua za haraka ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kutokana na
ongezeko kubwa la mfumuko wa bei uliopo sasa.
Mbunge huyo
aliyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo
alisema hali ngumu ya maisha iliyopo sasa inatokana na mfumuko wa bei
na kuporomoka kwa sarafu hali ambayo ni tishio kwa uchumi na wa nchi na
maisha ya wananchi.
Alisema serikali inapaswa kutambua mfumuko
wa bei uliopo sasa ni kama janga kwa taifa kwani hali hiyo inasababisha
wananchi kuishi katika hali ngumu jambo ambalo linaweza kuchangia
kushusha uchumi wa Taifa.
“Kwa sasa mfumuko wa bei umeongezeka
kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linafanya maisha ya watanzania kuendelea
kuwa magumu kwani wanashindwa kumudu bei za bidhaa hali inayozidi
kuwasababishia ugumu wa maisha,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba
“Kwa
sasa serikali inatakiwa kulichukulia jambo hili kama dharura kwa
kupeleka mpango wa dharura bungeni ili wabunge waweze kujadili na
kulitolewa maamuzi ambao utasaidia kupunguza ugumu wa maisha kwa
masilahi ya watanzania na kwa taifa ,” alisema
Alisema mfumuko
wa bei ulipo nchini unasababishwa kupunguza uzalishaji wa bidhaa za
ndani jambo ambalo kwa taifa linaweza kuleta madhara makubwa kiuchumi.
“Uchumi
wa taifa unaweza kuporomoka kwa kiasi kikubwa kama jambo hili la
mfumuko wa bei halitapewa kipaumbele kwani kwa sasa udhalishaji wa
bidhaa za ndani unapungua hasa kwa bidhaa zinazotokana na kilimo,”
alisema.
Alisema serikali inapaswa kuangalia kwa umakini matumizi
ya fedha za serikali pamoja na kuporomoka kwa sarafu kunatokana na
ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni pamoja na uagizaji wa mafuta na
malighafi nyingine toka nje jambo ambalo ilitawezesha kupunguza
mfumuko wa bei .
Kwa mujibu wa ripoti ya bei za bidhaailiyotolewa
na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) inaonyesha kwamba mfumuko wa bei
nchini kuanzia Disemba 2011 umeongezeka hadi kufikia asilimia 19.8
ikilinganisha na asilimia 19.2 Novemba 2011
No comments:
Post a Comment