Sio lengo langu kuwafundisha wanawake namna yakuachana na wapenzi au waume zao. Lakini hebu fikiria kwamba kila wakati wanandoa au wapenzi wako kwenye vita. Hakuna amani, hakuna masikilizano. Kutwa nzima mtu anawaza kuhusu uhusiano wake mbaya hadi anashindwa hata kufanya kazi. Je, hali kama hii ina maana kwa mtu kuendelea kuwa kwenye ndoa?
Hapa
nazungumzia wale ambao wanashindwa kutoka kwenye uhusiano, ambao
wanajua kabisa kwamba, unawatesa na kuwaumiza. Kuna sababu nyingi kwa
nini watu hawa wanashindwa, lakini nyingine zinatokana tu na kutojua
namna ya kutoka, sio utegemezi wa aina yoyote.
Moja
ya sababu, ambazo ninaziona sana hasa kwa wanawake ni kujali jamii
itasemaje. Mtu anaona kabisa uhusiano haufai na anatamani kutoka .
lakini anajiuliza, hivi watasemaje? Kuna wakati ndugu wanamwambia, yeye
ndiye mkorofi. Kama hii ndio sababu anachotakiwa kufanya mwanandoa ni
kuhakikisha kwamba anajifunza kuishi kama yeye. Nijuavyo mimi, hata
wanandugu au jamii hata ikisema vipi, anayeumia au kuepuka kuumia au
kuuawa ni yule aliye kwenye mateso ya ndoa
Jambo
la kujiliza hapa ni kama, jamii ndiyo inayopigwa, kutukanwa,
kutelekezwa au kudhalilishwa? Lakini jambo kubwa zaidi la kufahamu ni
kwamba mtu alishaolewa maana yake ni mtu mzima mwenye haki ya kuamua juu
ya maisha yake. Akisbiri ndugu wamwamulie, basi huyo bado ni mtoto..
Jambo
lingine ni lile la, je nikimwacha nitapata mwingine? kwani wanaume siku
hizi ni shida sana? Ni ujinga unaowafanya wengi kuuliza swali hilo.
Unahitaji mwingine wa nini? Unahitaji mwingine ili maisha yako yawe ya
maana zaidi au? Kama hakuna mwingine ni vyema kwa sababu maana yake ni
kwamba hakuna mwingine wa kukutesa. Lakini wanasaikolojia wanaamini
kwamba, ‘kila bidhaa ina mnunuzi.’ Kama unataka mwingine, hata ukiwa na
miaka sitini utampata. Huwezi kumpata wakati ukiwa ndani ya tanuru la
mateso. Ni lazima utoke kwanza.
Kuna
wale wanaoshindwa kutoka kwa sababu wanaamini kwamba mwanamke
haruhusiwi kutoa talaka. Hi siyo kweli. Kuna wanaoshindwa kutoka kwa
sababu dini zao zinakataza kuachana, hii pia siyo kweli. Mwanamke au
mwanaume, yeyote anaweza kuomba talaka na ikatolewa, kama kuna sababu
zenye kukidhi haja hiyo. Chombo pekee kinachoweza kutoa talaka au
kuidhinisha wanandoa kuachana ni Mahakama, siyo dini au taasisi
nyingine. Kinachoitwa ‘talaka tatu’ kwa mfano, ni ushahidi tu, na sio
talaka.
Kuna
wale ambao hawako tayari kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu ya
mali. Wanaogopa watagawana mali na wenzao, jambo ambalo hawako tayari
kulifanya na mara nyingi hawa ni wanaume. Wapo pia wanawake ambao wao
ndio waliokuwa watafutaji wakuu. Swali la kujiuliza ni hili. ‘Ni kipi
bora, ni mali au ni amani na utulivu na uhai wako?’ kama ni mali, basi
hakuna anayeweza kukuingilia kwenye uamuzi wako.
Lakini, kwa ufahamu tu, ni kwamba, pasipo na amani, mali haina maana na pasipo na amani uhai ni wa kubahatisha pia.
Wengine
wanashindwa kutoka kwenye husiano kwa sababu wazazi wa mume na ndugu
wanampenda sana. Anaogopa kuwaudhi kwa kuondoka kwenye ndoa ya mateso ya
mtoto wao na ndugu yao. Anataka wafurahi, hivyo hawezi kuondoka. Huu
nao ni upungufu.
Hivi
unakuwa umeolewa na ndugu na wazazi au na mume? Lakini, kwani ukiondoka
utashindwa kuwa karibu na watu hawa? Hutashindwa na pengine urafiki
wenu utakuwa wa kudumu. Ukiendelea kukaa kwenye ndoa ya mateso kuna siku
utakosana hata na hawa, maana unaweza ukalipukwa ukamuuwa mtoto au
ndugu yao.
Kuna
wale wanaoshindwa kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu wana watoto
na wanaogopa kwamba, watoto wao watateseka. Hivi ni kuteseka kupi
kubaya, kule kwa utotoni au ukubwani? Mtoto anayeishi kwenye ndoa yenye
vurugu, anaharibikiwa kuanzia utotoni hadi ukubwani. Lakini, hata hivyo
kuachana kwa wazazi, sio lazima kuwe na maana ya watoto kuteseka.
Kuna
wakati hata watoto wanamwambia mama atoke kwenye ndoa, halafu mama huyo
huyo anadai anakaa kwenye ndoa hiyo kwa sababu ya watoto! Kuna haja ya
kujiuliza maswali kwa upana zaidi.
Ukitaka
kutoka kwenye ndoa ngumu jiulize maswali haya. Je, ndoa hii ni kwa
faida ya nani? Je, niliolewa au kuoa ili kupata shida au amani na
upendo? Je, bila ndoa,nisingeweza kuishi mwenyewe? Tafuta mifano ya
wasio na ndoa ambao wanafurahia maisha.
Jiulize ni kwa kiasi gani wengine wanasaidia kukusukuma zaidi kwenye ndoa hiyo? Jiulize ukamilifu wako. Je, wewe ni nusu mtu au mtu kamili? Kama ni mtu kamili , basi ishi kama mtu kamili.
No comments:
Post a Comment