NJOMBE

NJOMBE

Thursday, February 2, 2012

Wanafunzi 875 wakatiza masomo kwa mimba

WANAFUNZI 875 wa shule za msingi na sekondari mkoani Tabora, walikatisha masomo kwa kipindi cha miaka minne kutokana na kubeba ujauzito.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu Msaidizi huduma za jamii na Ofisa Elimu wa mkoa huo, Paul Makungu, alisema kwa kipindi hicho, wanafunzi wa shule za sekondari waliopata ujauzito ni 388 na msingi ni 487.
Akifafanua zaidi alisema kuwa kwa mwaka 2008, waliopata ujauzito kwa shule za msingi walikuwa 85, mwaka 2009 walikuwa146, mwaka 2010 ni 107 na kwa mwaka jana ni wanafunzi 163.
Makungu alisema kwa upande wa sekondari, waliopata mimba ni 38 kwa mwaka 2008, wakati mwaka 2009 walikuwa 68, mwaka 2010 walikuwa 88 na mwaka jana ni 194.
Wilaya zilizoongoza kuwa na wanafunzi wengi waliobeba ujauzito ni Nzega na Urambo. Na kwamba kuna kesi 18 mahakamani za wanafunzi na kesi 165 bado zipo ngazi ya kamati za shule na kesi 135 zipo katika ngazi ya serikali za kata na vijiji.

No comments:

Post a Comment