NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

TAACINE, TPN wawaangukia madaktari

CHAMA cha Waajiri wa Mashambani, Viwandani, Biashara na Madini (TAACIME) na Mtandao wa Kitaaluma Tanzania (TPN), wamewaangukia madaktari wakiwataka wasitishe mgomo wao na kurejea kazini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, kaimu mwenyekiti chama hicho, Anthony Teye, alisema kuwa mgomo huo ni batili kwani haujafuata sheria ya kazi ya mwaka 2004 namba sita.
Teye aliwataka madaktari hao kurejea kazini ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa ili kuepusha vifo kwa raia wasio na hatia.
Aidha Teye alisema kuwa kila daktari azingatie kiapo cha taaluma na kukumbuka kuwa waligharamiwa na umma hadi kufuzu kwao.
Wakati huohuo, rais wa TPN, Phares Magesa, amewapa pole Watanzania waliokumbwa na madhara yaliyotokana na mgomo, akisema kuwa ili serikali iweze kukabiliana na tatizo hilo mapema kuna haja ya kufanya mazungumzo na madaktari wakati ikijiandaa kutekeleza ahadi zake.
Hata hivyo aliwataka madaktari wote kurejea maeneo yao ya kazi wakati madai yao yakishughulikiwa na wafanya kazi kwa kujali maisha ya binadamu.
Pia aliitaka serikali kuangalia upya uamuzi wa awali wa kuwafukuza kazi wale madaktari ambao walikuwa bado hawajaripoti kazini badala yake itafute hatua nyingine za kinidhamu.

No comments:

Post a Comment