NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, February 21, 2012

Maafa Makubwa Bunda kutokana na Mvua

ZAIDI ya watu 80 katika Kijiji cha Serengeti katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, hawana mahali pa kuishi, baada ya nyumba zao kuezuliwa kwa upepo mkali, ulioambatana na mvua kubwa.Diwani wa Kata ya Kunzugu inayojumuisha kijiji hicho, Ndovu Chacha, alisema upepo na mvua hiyo ulivuma juzi jioni na kwamba licha ya kuezua nyumba, pia umeharibu mazao ya mashambani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Serengeti, Yombi Msagasa, alisema nyumba zilizoezuliwa na upepo huo ni         Mnara wa Tigo ulioanguka kutokana na mvua kubwa mkoani Bunda.                                                                                                          na kwamba sita miongoni mwa hizo, ziliezekwa kwa kutumia nyasi.Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kijiji, nyumba nyingine 25 zilizokuwa zimeezekwa kwa mabati.

Imeelezwa kuwa kwa sasa watu ambao nyumba zao zimeezuliwa, wanahifadhiwa  na ndugu, jamaa na majirani zao.Diwani Ndovu alisema tathimini kuhusu  hasara kamili iliyosababishwa na mvua hiyo inaendelea kufanyika.

“Bado tunafanya tathmini ili kujua hasara kamili iliyosababishwa na mvua hiyo, lakini hali ni mbaya sana maana watu hawana mahali pa kuishi” alisema Diwani huyo, kwa njia simu.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa wilayani humo, alisema  bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.Hata hivyo alisema atalifuatilia
ZAIDI ya watu 80 katika Kijiji cha Serengeti katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, hawana mahali pa kuishi, baada ya nyumba zao kuezuliwa kwa upepo mkali, ulioambatana na mvua kubwa.Diwani wa Kata ya Kunzugu inayojumuisha kijiji hicho, Ndovu Chacha, alisema upepo na mvua hiyo ulivuma juzi jioni na kwamba licha ya kuezua nyumba, pia umeharibu mazao ya mashambani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Serengeti, Yombi Msagasa, alisema nyumba zilizoezuliwa na upepo huo ni 31 na kwamba sita miongoni mwa hizo, ziliezekwa kwa kutumia nyasi.Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kijiji, nyumba nyingine 25 zilizokuwa zimeezekwa kwa mabati.

Imeelezwa kuwa kwa sasa watu ambao nyumba zao zimeezuliwa, wanahifadhiwa  na ndugu, jamaa na majirani zao.Diwani Ndovu alisema tathimini kuhusu  hasara kamili iliyosababishwa na mvua hiyo inaendelea kufanyika.

“Bado tunafanya tathmini ili kujua hasara kamili iliyosababishwa na mvua hiyo, lakini hali ni mbaya sana maana watu hawana mahali pa kuishi” alisema Diwani huyo, kwa njia simu.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa wilayani humo, alisema  bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.Hata hivyo alisema atalifuatilia
Habari na Mwananchi

No comments:

Post a Comment