Akizungumza na katika Mahojiano na Magic FM asubuhi jana Ngeleja alisema kinachoongelewa na Zitto ni nadharia kutokana na fedha hizo hazijathibitishwa na mtu yeyote.Alisema Kuna matatizo ya ubadhirifu katika Wizara lakini sio kwa kiasi hicho anachokisema kutokana na kwamba hakuna kiongozi yoyote aliyethibitisha.
Alisema kama kuna mtu aliziiba fedha hizo basi Serikali ina mkono mrefu wa kuhakikisha inawakamata wale wote walio husika. Ngeleja alisema Zitto alisema jambo hilo kisiasa kutokana na kwamba hakutoa kidhibiti chochote kilichoonyesha kuna upotevu wa fedha hizo.
“Hakuna upotevu huo, kinachosemwa na Zitto Kabwe ni nadharia tu,” alisema Ngeleja.
Zitto aliibua upotevu wa wa Sh2.7 trilioni katika sekta ya madini, kutokana na ukaguzi uliofanywa kwenye sekta hiyo na mwaka jana na Wakala wa Ukaguzi wa sekta ya madini (TMAA).

Alisema baada ya kugundua utata huo anaomba wabunge kuundwa kamati ili kuweza kuangalia sekta zingine ikiwemo sekta ya gesi na mafuta ambazo zinalalamikiwa na wabunge kupoteza fedha nyingi.
Hata hivyo Ngeleja alisema Serikali imekuwa makini kila kukicha kuhakikisha rasilimali za Taifa zinatumika kama iklivyokusudiwa na kwamba , Serikali haitaweza kuvunja mkataba kutokana na kwamba kunahitaji kukaa chini na kuweza kutafakari pamoja na kushirikisha tume ya Usuluhishi.
Alisema inawezekana kuna watendaji wabovu katika Wizara ambao tunaweza kuwaita wahalifu lakini sio kwa kiasi hicho alichokiongelea mheshimiwa Zitto.
Ngeleja alisema kutokana na matatizo yaliyokuwa yanalikumba Taifa ya uhaba wa umeme kwasasa kuna akiba ya umeme wa Megawati 300 baada ya kuzalisha Megawati 1028 huku matumizi yakifikia 720 kwa jana.
Alisema kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha umeme bado Wizara haijakaa kimya bali inashirikiana na Tanesco kuhakikisha utegemezi wa nishati ya maji unapungua .
Alisema baada ya kujua nchi inahitaji umeme kwa wingi ndio ikaamua kuingia katika mikataba ya dharura lakini mikataba hii ndio inayowatesa watanzania kwa sasa kutokana na kwamba gharama za uzalishaji nazo hupanda.
Alisema kwa kiasi kikubwa Gharama ya umeme kwa watanzania ni kubwa klakini kutokana na hatua hiyo, Serikali imeamua kufanya jambo hili kwa mda wa miezi sita na kwamba kama kutakuwa na marekebisho Serikali itapunguza.
“Gharama hizi za upandishaji umeme hufanyiwa baada ya miezi sita, ndio maana tunasema ni za mpito licha ya kwamba zinawatesa sana watanzania” alisema Ngeleja. Aliongeza kwamba Serikali imeaza kutoa vibali kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini ili kuweza kupewa leseni.
Ngeleja alisema kutokana kwamba wachimbaji wadogo kuanza kupewa leseni , Serikali imeamua kuweka vituo vya kuwasaidia wachimbaji wa madini ili kupata vifaa vya kisasa. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni pamoja na kituo kilichopo Tanga, Mwanza, Arusha ili kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo.
Alisema kutokana na changamoto mbalimbali za uchimbaji , aliwataka wafanyabishara wakubwa wenye uwezo kuweza kujenga kituo cha kusafishia madini hapa nchini ili kutowa usumbufu
No comments:
Post a Comment