Jaji Mwanahamisi Kwariko.
Nathanel Limu.
Mahakama
kuu kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini Singida
imemwamuru mshitakiwa Simon Andrew mkazi wa kijiji cha Kidaru wilayani
Iramba, kupelekwa kwenye taasisi inayojishughulisha na magonjwa ya akili
kwa kipindi chote cha maisha yake yaliyobakia hapa duniani.
Akitoa
amri hiyo, Jaji Mwanahamisi Kwariko amesema mahakama yake imekubaliana
na upande wa mashitaka kwamba mshitakiwa Simon alimuua bibi kizee Tiale
Mbogo kwa kukusudia.
Aidha,
Jaji Kwariko amesema mahakama pia inakubaliana na upande wa mashitaka
kwamba wakati mshitakiwa Simon akitenda kosa hilo hakuwa na akili
timamu.
“Mahakama
hii imepokea ripoti kutoka kwa daktari kuwa mshitakiwa ni mgonjwa sugu
wa afya ya akili, Kwa hali hiyo, mahakama imefiakia uamuzi kuwa
mshitakiwa Simon apelekwe kwenye taasisi inayojishughulikia watu wenye
magonjwa ya akili”,amesema.
Awali
mwanasheria mkuu wa serikali Neema Mwanda, alidai mbele ya Jaji Kwariko
kuwa mnamo Desemba 18 mwaka 2000 katika muda usiofahamika, mshitakiwa
alimuuwa kwa makusudi kikongwe Tiale Mbogo.
Neema amesema kuwa mshitakiwa Simon alikutwa na majirani wa bibi kikongwe Tiale akiwa amesimama jirani na mwili wa Tiale.
Watu hao waliweza kumkamata mshitakiwa na kumfikisha mbele ya vyombo vya dola.
Imedaiwa
bibi Tiale kabla ya kufikwa na mauti hayo, alikuwa akiota jua.
Mshitakiwa alimpiga na kitu ambacho hakijafahamika na kisha kufariki
dunia papo hapo.
No comments:
Post a Comment