Katibu
tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akifungua mafunzo ya siku moja
yaliyohudhuriwa na kamati ya seketarieti ya mkoa wa Singida na za
halmashauri za wilaya ya Manyoni na Singida.
Mshauri
mwandamizi wa Mrogramu ya usambazaji wa maji vijijini RUWASA-CAD
Kazuyuki Suenaga akitoa taarifa yake mbele ya mkutano wa mafunzo
yaliyohudhuriwa na kamati za maji na usafi wa mazingira ya seketarieti
mkoa wa Singida na za halmashauri za wilaya ya Singida na Manyoni.
Baadhi
ya wanakamati za maji na usafi wa mazingira za seketarieti ya mkoa wa
Singida na halmashauri za Manyoni na Singida.(Picha zote na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu.
Katibu
tawala mkoa wa Singida Liana Hassan amesema programu za maji
zinazofadhiliwa na wafadhili mbali mbali, zitakuwa endelevu tu iwapo
zitasimamiwa na watu waliofunzwa vema mbinu bora za uendeshaji wa miradi
ya maji.
Akifungua
mkutano wa siku moja wa kwanza uliohusu mafunzo ya kuzijengea uwezo
timu za maji na usafi wa mazingira za sekretarieti ya mkoa na zile za
halmashauri za wilaya ya Manyoni na Singida, Hassan amesema mafunzo hayo
yanalenga kuzijengea uwezo timu hizo ili ziweze kusimamia vizuri
utekelezaji wa usambazaji wa maji vijijini awamu ya pili (Rural water
supply and sanitation capacity development -RUWASA – CAD).
AKifafanua
amesema watu/viongozi hao waliofunzwa vema juu ya uendeshaji bora wa
miradi ya maji, watasaidia kuwafunza na kuwahamasisha watumiaji wa
maji, mbinu sahihi zitakazosaidia miradi yao ya maji, kuwa endelevu.
Aidha,
Katibu huyo wa mkoa amesema lengo letu sote ni kuhakikisha kuwa
asilimia 48 ya wakazi wa mkoa wa Singida wanapata maji safi na salama
kwa umbali mfupi kutoka wanakoishi.
Lengo hilo litafikiwa tu iwapo jamii itakuwa imeelimishwa mbinu ya kutunza miradi hiyo.
Katika
hauta nyingine, Katibu tawala huyo amesema utekelezaji wa mradi wa
usambazaji wa maji vijijini utakapoanza, uangalie uwezekano wa kusaidia
kugharamia masomo ya ufundi wa pampu za maji na injini kwa vijana
waishio vijijini, ili kuondoa uhaba mkubwa wa mafundi wa aina hiyo ngazi
ya vijiji.
Kwa
upande wake mshauri mwandamizi wa mradi wa RUWASA – CAD awamu ya pili
Kazuyuki Suenaga, amesema kwa sasa wanaendelea kuzijengea uwezo timu za
maji na usafi wa mazingira za sekretarieti ya mikoa na za halmashauri za
wilaya.
Suenaga
asema timu hizo za mikoa ya Singida, Tabora na Mwanza, zitajengewa
uwezo kwa kupatiwa mafunzo yanayohusu uendeshaji na utunzaji bora wa
miradi ya maji.
Amesema
wanayo imani kwamba baada ya kuzifunza timu hizo na zenyewe, zitafunza
jamii ili miradi iliyopo kwenye maeneo yao iwe endelevu.
Aidha,
Suenaga amesema kutokana na hitaji la Tanzania la uboreshaji wa sekta
ya maji, serikali ya Japan imeamua kuiunga mkono kwa kusaidia
kupatikanaji wa maji safi na salama na usambazaji wake, maeneo ya
vijijini chini ya ushirikiano na program ya Japan International
Co-operation Asency (JICA).
No comments:
Post a Comment