Katibu mtendaji wa baraza la
Taifa la mitihani Tanzania (NECTA), Dkt Joyce L. Ndalichako ameeleza
kuwa jumla ya wanafuzi 3303 wamefutiwa mitihani yao kutokana na
kuthibitika kufanya udanganyifu.
DK. Joyce liyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Bwawani mjini zanzibar.
Aliongeza
kuwa kati ya hao kuna baadhi ya watahiniwa wameandika matusi katika
karatasi zao kamitihani na wengine kuwacha maswali na kutokujibu kabis maswali ya majibu hayo. Hata hivyo Dkt Joyce alishindwa
kujibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kutokana na kutokufanya
majumuisho yote ya mitihani hiyo iliyofanyika nchini.
Aidha
alieleza kuwa suwala hilo la udanganyifu linafanyika katika makundi
yote matatu ambao ni walimu wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe.
Dkt Jooyce ameongeza kuwa waliofutiwa mitihani kulitokana na kikao cha 86 nambari
6 B kilichofanyika tarehe 7-2-2012. Kanuni za baraza la mitihani
zinazoeleza kuwa watahiniwa hao hawataruhusiwa kufanya mitihani kwa muda
wa miaka mitatu.
Hata hivyo amesema kuwa baraza limewaonea huruma kwa kuwapa hukumu hiyo kwani katika kanuni za NECTA wanafunzi wanaofutiwa mitihani hawaruhusiwi kufanya mitihani tena.
Pia
katibu mtendaji huyo aliwataka wasimamizi kuwa makini katika kazi zao
na kusimamia kwa uwangali mitihani kwani udanganyifu huwa unamadhara
makubwa katika taifa ambapo kutazalishwa wataalamu wasio na viwango hasa katika kipindi hiki ambapo tunaingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati
huo huo chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewasimamisha
wanafunzi watatu wa chuo hicho baada ya kubainika walitumia vyeti vya
kughushi wakati walipojiunga na chuo hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika chuo hicho, Vuga mjini Zanzibar,
mwanasheria wa SUZA Mtaibu Abdalla Othman amewataja wanafunzi hao kuwa
ni Mahfoudhat Hassan Khamis anaesoma digrii ya sanaa, Shafii Suleiman
Mringo anaesoma cheti cha teknolojia ya habari na Yussuf Khamis anaesoma
cheti cha sayansi ya komputa.
No comments:
Post a Comment