NJOMBE

NJOMBE

Saturday, February 4, 2012

Mgawo wa umeme wawaliza

Habari na Clever Perfect,Songea
UBOVU wa mashine tatu za kuzalishia umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha mjini hapa mkoani Ruvuma umesababisha mgawo wa umeme hali inayosababisha malalamiko kwa wananchi.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu, umebaini kuwa mgawo huo umesababisha kazi za kiuchumi kushindwa kufanyika na kusababisha baadhi ya wananchi wenye uwezo kutumia majenereta madogo huku maeneo mengi ya mji yakiwa giza kwa saa kadhaa nyakati za usiku.
Kaimu mkuu wa kituo cha kuzalishia umeme mjini hapa Isaack Mbata alikiri mgawo huo kusababishwa na ubovu wa mashine hizo tatu zenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.2.
Alisema mashine tatu zinazozalisha umeme hivi sasa katika mji wa Songea zina uwezo wa kuzalisha megawati 2.2 wakati mahitaji halisi ya umeme katika mji huo ni megawati 4.5.
“Umeme unaozalishwa hivi sasa ni karibu nusu ya mahitaji ya umeme katika mji wa Songea, hali hii imesababisha kuwepo mgawo mkali wa umeme, hata hivyo vipuli vya mashine tatu ambazo ni mbovu vimeagizwa na Tanesco makao makuu na vitakapoletwa tutavifunga mara moja na umeme utarudi katika hali yake ya kawaida,’’ alisema Mbata.
Naye Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Ruvuma, Haruna Mwachula, amewaomba wakazi wa mji wa Songea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho shirika hilo linafanya juhudi za kutengeneza mashine hizo ili kupunguza mgawo mkali wa umeme uliopo.
Alisisitiza kuwa mafundi wa TANESCO wanafanya kazi usiku na mchana ambapo tayari wamefanikiwa kufungua vipuli vyote vibovu kwenye mashine aina ya Katapila na ABC zenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.2

No comments:

Post a Comment