NJOMBE

NJOMBE

Sunday, February 5, 2012

Waislamu watakiwa kupinga tawala za mabavu duniani

WAISLAMU wametakiwa kuunganisha nguvu kwa pamoja katika kupinga tawala za mabavu duniani, zisizopenda kusimamia haki za binadamu.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran, Morteza Sabouri, katika wiki ya maadhimiiisho ya siku ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Mfalme Shahah mwaka 1979.
Alisema Wairani wakiwa chini ya kiongozi wao, Imam Ayatollaha Khomeni wamefanikiwa katika hatua mbalimbli baada ya kuungana na kuelewa wanataka nini ndipo walipoamua kufanya mapinduzi yaliouangusha utawala huo wa kidhalimu wa Shahah.
Sabouri alisema mapinduzi hayo yameleta mwanga kwa wananchi baada ya mapinduzi, ikiwa ni miaka 33 tangu yatokee.
Alisema kutokana na mshikamano pamoja na uzalendo uliyojengeka kwa wananchi wa nchi hiyo umeweza kusaidia nchi hiyo kupiga hatua kimaendeleo hasa katika nyanja ya kiteknolojia hali inayowatisha Wamarekani.
Alisema Imam Khomeini alipinga mfumo wa matabaka hasa katika kuwabagua baadhi ya watu na kuwaweka katika daraja la juu na wengine kudharauliwa.

No comments:

Post a Comment