HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), inatarajiwa kukutana kwa
dharura mjini Dodoma Februari 12 mwaka huu.Kikao hicho cha Nec kinakuja
kipindi ambacho upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho tawala umekuwa
ukivuma vibaya, kufuatia wabunge wake kuingia katika vita ya chini chini
na Serikali yao inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa
zilizopaatikana jana kutoka ndani ya CCM, zilisema tayari wajumbe wa Nec
wamekwishafahamishwa kuwapo kwa kikao hicho cha dharura.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, pamoja na mambo mengine, kikao hicho cha Nec
kitajadili masuala ya mchakato wa Katiba ya chama hicho.
Taarifa
hizo zilifafanua zaidi kwamba, wajumbe watajadili jinsi ya kuwapata
wajumbe wa Nec upande wa Zanzibar, baada ya katiba ya chama hicho
kufanyiwa marekebisho kuhusu taratibu za kuwapata wajumbe hao.
Kauli Nape
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alithibitisha kuwapo kwa
kikao hicho cha Nec na vingine vya chama hicho tawala lakini, akisema si
vya dharura.
Nape alisema leo kutakuwa na kikao cha Sekretarieti ya chama hicho itakayokutana mjini Dodoma.
Kamati ya Maadili
Alitoa
ratiba ya vikao hivyo akisema, Februari ya 11 mwaka huu kutakuwa na
kikao cha Kamati ya Maadili asubuhi na kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu
(CC) baadaye mchana.
Katibu huyo aliongeza kwamba, Febrauri 12
kutakuwa na kikao cha Nec huku ajenda kuu ikiwa ni kupitia mabadiliko ya
katiba ya chama ili kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi.
"Tunafanya hivyo kwakuwa kuna watu walikuwa wanahoji uchaguzi
utafanyikaje wakati Nec haijakaa, kwa hiyo hiki ni kikao maalumu cha mabadiliko ya katiba ili uchaguzi ufanyike, " alisema Nape.
CCM
imeanza mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama hicho ambao
uchukuaji wake wa fomu ulianza Februari 4 mwaka huu huku uchaguzi
ukitarajiwa kuendelea awamu kwa awamu, kuanzia jumuiya na chama hadi
Juni.
Vikao hivyo vya juu vya chama vinafanyika wakati pia chama
hicho kikiwa bado hakijatekeleza mpango wa kujivua gamba ambao kwa sasa
ulirudishwa CC kwa ajili ya maamuzi ya mwisho.
JK alivyowalainisha
Hata
hivyo, juzi Rais Kikwete alifanikiwa kuwalainisha wabunge hao wa CCM,
ambao walikuwa wameweka msimamo wa kukataa Muswada wa Marekebisho ya
Mabadiliko ya Katiba.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na
wabunge wachache, walikubali kupitisha muswada huo ambao unatarajiwa
kuwasilishwa bungeni leo.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao
hicho ni Jenister Mhagama (Peramiho), Peter Selukamba (Kigoma Mjini),
Angela Kairuki (Viti Maalumu), Anna Kiliango (Same Mashariki), Saidi
Nkumba (Sikonge), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro) na Muhammad Amour
Chomboh (Magomeni).
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, wabunge
hao walifikia uamuzi huo baada ya Rais Kikwete kuwaeleza kwamba bado
wanayo nafasi ya kufanya marekebisho wanayoona yanafaa, kwa sababu
yaliyopelekwa na Serikali ni mapendekezo.
“Kwa kweli tumemwelewa
Rais, mwanzo kuna vitu ambavyo vilikuwa hatujaelezwa vizuri. Rais
alichotwambia ni kwamba sisi ndiyo waamuzi wa mwisho, Serikali imeleta
mapendekezo tuna haki ya kufanya marekebisho kwa sababu hiyo ndiyo kazi
yetu,” alisema mmoja wa wabunge hao na kuongeza:
“Rais ametwambia
hakuwa na makosa kukutana na Chadema, amekutana nao kama alivyofanya
kwa makundi mengine, na mapendekezo yao amatuletea sisi ndiyo waamuzi
tupime wenyewe.”
No comments:
Post a Comment