Mwandishi Wetu, Bagamoyo
WANAFUNZI wanane wa Shule ya Sekondari
Bagamoyo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo kujibu
tuhuma za kumbaka mwalimu wao kwa zamu.
Katika kesi hiyo
iliyojaza umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo, imedaiwa kuwa wanafunzi
hao walimbaka mwalimu huyo kwa zamu na kumsababishia maumivu makali.
Mwendesha
Mashtaka wa Polisi, William Mwantela alimwambia Hakimu Mkazi wa
Mahakama hiyo, Said Mkasiwa kuwa wanafunzi hao walitenda kosa hilo
Januari 16 mwaka huu katika mazingira ya shule hiyo.
Aliwataja
wanafunzi hao kuwa ni Emmanuel Antoni, Fadhili Nassoro, Nassa Yohana,
Benjamini Mhina, Yusuph Timothy, Frank Jackson, Frank Kanya na Hamisi
Timbwa.
Mwendesha mashtaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa
tukio hilo lilitokea shuleni hapo Januari 16 mwaka huu majira ya saa
9:00 jioni.
Hata hivyo, watuhumiwa hao wote walikana shtaka na
kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 29 mwaka huu baada ya mwendesha
mashtaka huyo kudai kuwa ushahidi haujakamilika.
Awali kabla ya
kuahirisha kesi hiyo upande wa utetezi ulimwomba hakimu kuruhusu dhamana
na hakimu aliruhusu akitaka kila mmoja adhaminiwe na mtu mmoja mwenye
hati na kitambulisho ambaye atasaini hati ya dhamana ya Sh2milioni.
Washitakiwa
watatu walifanikiwa kutimiza masharti hayo ya dhamana na wako nje,
lakini wengine watatano wameshindwa na kupelekwa rumande hadi kesi hiyo
itakapotajwa tena siku iliyopangwa.
No comments:
Post a Comment