WANANANCHI WA KIGOMBE WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA. WA KWANZA KULIA NI MSAIDIZI WA MKUU WA MKOA BW. JOSEPH SURA. |
BOTI YENYEWE AMBAYO IMECHOMWA MOTO NA MAHARAMIA |
MKUU WA MKOA WA TANGA MH GALLAWA AKIWA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MUHEZA NA KIJIJI CHA KIGOMBE WALIPOMTEMBEZA KWENYE MWAMBAO WA PWANI KUONA ENEO LILILOHIFADHIWA KWA AJILI YA SAMAKI AINA YA SILIKANTI. |
MAHARAMIA wanaoendesha uvuvi haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi mkoani Tanga, wameichoma moto boti ya doria inayomilikiwa na Taasisi ya Hifadhi ya bahari ya Silikanti iliyopo katika kijiji cha Kigombe wilayani hapa.
Kuchomwa
kwa boti hiyo iliyokuwa ikielea baharini katika eneo hilo la Kigombe,
kunatokana na dori ya mara kwa mara inayofanywa na taasisi hiyo kwa
ajili ya kuwasaka maharamia wanaoendesha uvuvi haramu wa kutumia mabomu
na nyavu ndogo zisizoruhusiwa, kumeelezwa kwamba ndiko kuliwapa hasira
maharamia hao, wakachukua maamuzi hayo.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kigombe Bew. Mwambi Haji alimweleza Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa aliyefika katika kijiji hicho
kupata maelezo ya kuchomwa kwa boti hiyo, alisema tukio hilo lilitokea
hivi karibuni na hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na
tukio hilo.
Mhifadhi
wa bahari ya Silikanti Bw. Sylevester Kazimoto alisema katika kipindi
cha mwaka uliopita waliendesha doria 192 za baharini na nchi kavu
iliyohusisha vyombo vya dola ambayo iliwezesha kukamatwa kwa wavuvi
haramu wapatao sita.
Alisema
pamoja na kuwakamata wavuvi hao pia walikamata vifaa vinavyotumika kwa
uvuvi huo ikiwemo baruti 29, bunduki 17 za kuulia samaki, mitungi 31 ya
kuzamia, makokoro 94, nyavu za utale 11 na samaki wa baruti kilo 124.
Akizungumza
katika mkutano na wananchi waliofika katika ofisi ya hifadhi hiyo Mkuu
wa Mkoa alisema kuwa kila wananchi analojukumu kubwa la kulinda na
kuhifadhi rasilimali za bahari hivyo akawataka wataalamu wa hifadhi hiyo
wakishirikiana na serikali ya kijiji kuandaa mpango wa kuorodhesha
wavuvi wote na boti zao kisha kuziandika namba.
Alisema
suala la uvuvi haramu hivi sasa linatakiwa kupigwa vita baada ya muda
mrefu nchi yetu kuliacha bila kuwachukulia hatua watu wanaoendesha uvuvi
haramu ambao licha ya kuharibu mazingira pia wanaleta matatiz ya kiafya
kwa kuvua samaki wa aina hiyo.
No comments:
Post a Comment