NJOMBE

NJOMBE

Monday, October 15, 2012

Wafanyakazi wa misaada watekwa nyara Niger

Hali ya njaa na magonjwa nchini Niger
Mashirika ya kutoa misaada nchini Niger yamesema kuwa takriban wafanyakazi wanne wa mashirika hayo wametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami.
Wafanyakazi hao kutoka Niger na Chad walitekwa nyara wakiwa mjini Dakro ambako walikuwa wakitibu wagonjwa wa Malaria na kuwasaidia watoto wanaokumbwa na utapia mlo.
Serikali ya Niger, imetuma wanajeshi kuwatafuta wafanyakzi hao.
Hata hiovyo haijulikani nani au kundi gani limefanya kitendo hicho.
Makundi ya kigaidi yenye uhusiano na Al Qaeda yamekuwa yakilaumiwa kwa visa vya awali vya utekaji nyara nchini Niger

No comments:

Post a Comment