NJOMBE

NJOMBE

clock

Monday, October 22, 2012

Ukombozi wa Bani Walid waendelea


Mamia ya watu wanaukimbia mji wa Bani Walid, ulioko kaskazini-magharibi mwa Libya, huku wapiganaji wa serikali wanaendelea kutumia mizinga na kusonga mbele dhidi ya ngome ya zamani ya Gaddafi.
Mji wa Bani Walid
Magari kadha yaliyosheheni watu na vitu vyao yalionekana yakikimbia kutoka mji huo uliozingirwa.
Wengine walionekana wakitembea kwa miguu.
Watu zaidi ya 20 walikufa kwenye mapigano mjini Bani Walid hapo jana.
Wapiganaji wa serikali wanasema wameazimia kuwatimua wafuasi wa Gaddafi kutoka mji huo.

No comments:

Post a Comment