NJOMBE

NJOMBE

Saturday, October 20, 2012

Mwaka mmoja baada ya kifo cha Gaddafi

Libya inaadhimisha mwaka mmoja baada ya aliyekuwa kiongozi wa nchi 
Wananchi wa libya wakiserehekea mwaka mmoja tangu kung'olewa kwa utawala wa Kanali Gaddafi
Wananchi wa libya wakiserehekea mwaka mmoja tangu kung'olewa kwa utawala wa Kanali Gaddafi
 hiyo Muammar Gaddafi kung'olewa madarakani na hatimaye kuuawa.
Gaddafi
Kanali Gaddafi alikuwa kiongozi aliyepigania Muungano wa nchi za Afrika akihimiza ushirikiano miongoni mwa mataifa hayo.
Hata hivyo kumeibuka maswali iwapo mshikamano wa Libya na mataifa mengine barani Afrika utaendelea baada ya kifo cha Gaddafi.
Gaddafi licha ya kuonekana kama dikteta, lakini pia alionekana kama mtu anayejali maslahi ya watu wake.
Mmoja wa wananchi wa Libya kutoka kabila la Tuareg Fnayet Al-Koni, anahisi kuwa utawala mpya wa nchi hiyo lazima uzingatie ushirikiano mpya na nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, tofauti na uhusiano ambao anautaja kuwa bandia kati ya Gaddafi na mataifa mengine ya Afrika.
Wananchi wa libya wakiserehekea mwaka mmoja tangu kung'olewa kwa utawala wa Kanali Gaddafi

No comments:

Post a Comment