NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 19, 2012

Wito wa kuhoji bajeti za nchi za ulaya

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, ametoa wito kwa Muungano wa Ulaya kuwezesha nchi wanachama kuwa na haki ya kuhoji bajeti ya taifa za nchi wanachama wengine
Bi Markel aliyasema hayo kwenye mkutano wa vingozi wa ukanda huo, waliokutana mjini Brussels kutafuta mikakati ya kumaliza msukosuko wa kifedha barani Ulaya.
Merkel pia aliwataka viongozi wenzake kutafakari kwa makini kuhusu sheria za utenda kazi wa benki, akisema kuwa ubora unapaswa kupewa kipaombele.
Ufaransa na Uhispania, zinataka mfumo mpya kuanza kutumika kuanzia Januari, tarehe mosi.
Uingereza ambayo ndiyo kitovu cha fedha barani Ulaya, inataka sheria zitakazoweza kulinda benki ya Uingereza.
Bi Merkel aliunga mkono wito wa waziri wake wa fedha Wolfgang Schaeuble, wa kutaka kamishna wa kusimamia sarafu ya Ulaya ambaye jukumu lake litakuwa kupiga kura ya turufu dhidi ya bajeti za nchi wanachama ikiwa zitavunja sheria za sarafu.

No comments:

Post a Comment