NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 12, 2012

Malema ahusishwa tena na ufisadi

Julius Malema
Mwanaharakati wa kisiasa nchini Afrika Kusini, Julius Malema, ameelezea kughadhabishwa na ripoti kuhusu madai ya ufisadi yanayohusisha kampuni anayoimiliki.
Alisema kuwa uchunguzi uliofanywa na mhifadhi wa mali ya umma, Thuli Madonsela kuhusu kampuni yake kupewa zabuni na serikali , ilimpata na hatia ya ufisadi bila yeye mwenyewe kuwepo.
Bi Madonsela alisema kuwa hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya kampuni hiyo.
Mwezi jana,bwana Malema alikanusha madai ya kujipatia pesa haramu ambazo zilihusishwa na kutolewa kwa zabuni za serikali.
Mwanasiasa huyo mwenye utata na ambaye amefurushwa kutoka chama tawala, kwa kuchochea migawanyiko chamani, alisema kuwa kesi hiyo imeshinikizwa kisiasa.
Katika ripoti yake, kuhusu kutolewa kwa zabuni za serikali, Bi Madonsela alidokeza kuwa zabuni ya huduma na usafirishaji wa bidhaa iliyotolewa na idara ya serikali ya barabara na usafiri katika mkoa wa Limpopo, kwa kampuni ya uhandisi ya On-Point Engineering, haikuwa halali.
Aliongeza kuwa Bbwana Malema na mshirika wake wa kibiashara wanaomiliki kampuni hiyo, walijinufaisha kwa vitendo fisadi vya kampuni yenyewe na idara ya usafiri ya serikali.
Ripoti ilisema kuwa kampuni hiyo ilishinda zabuni ya dola milioni 51 mnamo mwaka 2009 licha ya kwamba ilikuwa imeendesha shughuli zake tu kwa mwezi mmoja, haikuwa na wafanyakazi wala mali au kupata faida yoyote.

No comments:

Post a Comment