NJOMBE

NJOMBE

Wednesday, October 24, 2012

Wafungwa wapelekwa jela za mateso Urusi

Wanachama wawili wa bendi ya Kirusi ya Pussy Riot, ambao hivi maajuzi walifungwa kwa madai ya kumkejeli Rais Vladami Putin kutokana na nyimbo walioimba ndani ya kanisa la Othodox nchini humo,wamehamishwa hadi katika jela zinazosifika kwa mateso na kazi ngumu.
Wakili wao amesema Nadya Tolo-konnikova alipelekwa jela ya Mordovia, ilhali mwenzake Maria Alyo-khina katika jela la Perm, ambazo zote ziko Moscow.
Mashabikii wao wametuma ujumbe kupitia kwa mtandao wa Twitter wakilalamika kwamba jela walizohamishiwa ni mbaya zaidi
Mapema mwezi huu mwenzao wa tatu Yekaterina Samu-tsevich bila kutarajiwa aliachiliwa kutoka jela.

No comments:

Post a Comment